Loading...

ADHABU YA WABUNGE CHADEMA YALETA UTATA


MBOWE AMBANA SPIKA AELEZE KANUNI ILIYOTUMIKA.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani  Bungeni, Freeman Mbowe.
WAKATI wabunge sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakianza kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge la Bajeti vinavyoendelea mjini hapa, utata mkubwa umeibuka juu ya kanuni alizotumia Naibu Spika, Job Ndugai, kutoa adhabu hiyo.

Utata huo ulibainika jana wakati Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alipoomba mwongozo wa Spika Anna Makinda, kutaka kujua kanuni aliyotumia Ndugai wakati hakuna kanuni iliyomruhusu kutoa adhabu hiyo.


Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili jana pia walihoji kifungu kilichotumika hata kama wabunge hao walikosea.

Miongoni mwa waliohoji adhabu hiyo, wapo baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakupenda kutaja majina yao, wakisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika ulitawaliwa na jazba za kibinadamu badala ya kufuata kanuni zinazoliongoza Bunge.

Katika mwongozo wake jana kwa Spika Makinda, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani alihoji kifungu kilichotumika kuwaadhibu wabunge wake.

Mbowe alisema juzi wakati Bunge lilipokuwa katika kipindi chake cha jioni, wabunge sita wa CHADEMA waliotolewa nje kwa maelekezo ya Naibu Spika, Job Ndugai.

Aliwataja wabunge waliotolewa kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Haghness Kiwia (Ilemela), Ezekia Wenje (Nyamagana), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Pete Msingwa (Iringa Mjini).

“Na wabunge hawa walipotolewa, walipewa vile vile adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge, adhabu iliyotolewa papo kwa papo na Naibu Spika.

“Kwa mujibu wa kanuni zetu, kanuni inayompa Naibu Spika au Spika mamlaka ya kumtoa mbunge kwa siku tano ni kanuni ya 73 ya kanuni ndogo ya tatu ambayo inahusu mbunge ambaye atashindwa kutoa vielelezo vya aidha kusema uongo ambayo inasema hivi: 

“Endapo mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano,” alinukuu.

Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA, alisema yaliyotokea bungeni juzi ni sintofahamu kati ya wabunge na kiti cha Spika ambapo katika mambo ya msingi CHADEMA ilitegemea kifungu cha nne cha kanuni za Bunge, kifungu kidogo cha kwanza kingetumika.

Kifungu kinasema: “Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge.

“Ikiwa kwa maneno au vitendo, mbunge huyo anaonyesha dharau kwa Spika au atafanya kitendo chochote cha makusudi cha kudharau shughuli ya Bunge au mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.”

Kutokana na kanuni hiyo, Mbowe aliomba mwongozo wa Spika kutaka kujua wabunge hao walitolewa kwa kanuni gani na ni lini wataweza kurejeshewa haki yao ya kurejea ndani ya Bunge.

Vituko vya juzi
Baadhi ya askari walioamriwa kuingia ndani ya Bunge, walisema hawakuwa tayari kumtoa Lissu kwa nguvu ndio maana walitumia muda mrefu kutimiza agizo hilo.

Askari hao walisema hofu yao ilikuwa ni usalama wa Waziri Mkuu kwani endapo vurugu zingeibuka, angekuwa katika wakati mgumu kiusalama.

Baada ya Lissu na wabunge wenzake kutoka nje ya ukumbi chini ya ulinzi, askari hao walipata wakati mgumu kuwatoa nje ya eneo la Bunge.

“Tulipanda juu hadi kwenye ofisi ya Lissu, alipofika alikaa chini, akafungua kompyuta yake, baadaye akaizima wala hakuwa na haraka na sisi wakati huo tulibaki tumesimama tu.

“Baadaye aliizima, akachomoa waya  na kuziingiza kwenye begi lake, kisha alisimama taratibu na kuondoka kama vile hakuna jambo lililotokea,” alisema askari huyo.

Wenyewe wanena
Lema alisema: 
“Nimepokea kwa furaha adhabu hii kwa sababu imetokana na kupigania haki na ukweli ndani ya Bunge. Kwa hiyo adhabu hii kwangu ni baraka.”

Alisema uonevu wa wazi uliofanywa na Naibu Spika, Job Ndugai, baada ya muda kidogo Tanzania itashangilia ushindi mkubwa. Kwamba Watanzania watafurahia vijana wao na watoto wao walioshinda hofu.

“Ushahidi nilioombwa kuhusu mwenyekiti wa CCM kuwa mwasisi wa udini ninao, tena wa uhakika wa nguvu na imara na niko tayari kuutoa mbele ya Bunge kwa kuwa nilitoa maneno hayo mbele ya Bunge.

“Sitapeleka tena ushahidi wangu vichochoroni kwa kuwa nilipeleka ushahidi wangu kwa Spika kuhusu uongo wa Waziri Mkuu, walipiga chenga hadi wakanivua ubunge,” alisema.

Lema alidai kuwa ametumiwa meseji za vitisho kwamba wangelimuonyesha tena mahakamani, lakini akasema wafanye wafanyavyo ila moyo wake una furaha kuwa amesema yale ambayo wengine wameogopa kuyasema.

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, alisema: “Bunge letu lina matatizo, halina mwelekeo. Job Ndugai anajidai yeye ndiye kiongozi wa serikali.”

Alisema kama Ndugai ana sifa hizo na anajiandaa kuwa Spika wa Bunge lijalo, anamwomba Mungu asiwe mbunge katika Bunge hilo.

“Tusi lililotolewa na Peter Serukamba wa CCM, lilikuwa kubwa kuliko matusi yote yaliyowahi kutolewa ndani ya Bunge katika mabunge ya Jumuiya ya Madola.

“Hili lilihitaji adhabu, lakini kitendo cha Naibu Spika kumtimua Lissu ambaye alikuwa anafuata kanuni ni cha kusikitisha sana,” alisema.

Mbilinyi alisema wananchi wa Mbeya Mjini hawakumtuma kushangilia bungeni.

Kwa upande wake Mchungaji Msigwa alisema: “Adhabu hii ni ya hovyo kwa sababu haikufuata taratibu; wamegeuza Bunge kama sehemu ya serikali.”

Alifafanua kuwa kama angepata adhabu iliyofuata kanuni asingekuwa na shida, angeipokea kwa furaha.

“Naibu Spika ana jazba, anapaswa apate mafunzo ya jazba zake. Viongozi wa Bunge wamejaa u-CCM zaidi kuliko utaifa. Binafsi sitajali kufukuzwa, ninachotaka haki itendeke,” alisema.

Mbunge wa Ilemela, Kiwia, alisema adhabu waliyopewa ni kinyume cha kanuni.

“Adhabu hiyo anapaswa apewe mtu aliyesema uongo na kushindwa kuthibitishwa, pamoja na hayo kanuni zifanye kazi kwa wabunge kwa usawa,” alisema.

Kiwia aliongeza kuwa kanuni hazipaswi kuwaona wabunge wengine wana haki na wengine hawana; kwamba hoja za msingi zijibiwe, maamuzi bungeni yasifanyike kwa mabavu.

Naye Lissu ambaye ni mwanasheria kitaaaluma, alisema hajui ni kanuni gani iliyotumika na kumwadhibu na kwa kosa gani.
 

WANASONGEA WAILALAMIKIA MANISPAA KWA UBOVU WA KITUO KIKUU CHA MABASI


BAADHI ya abiria na wamiliki wamabasi katika halmashauri ya manispaa ya Songea wameulalamikia uongozi wa manispaa hiyo kwa kushindwa kukifanyia matengenezo kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea ambacho kimekithiri kwa kuwa na mashimo mengi na kusababisha magari yanayoingia na kutoka kuharibika yakiwa kwenye kituo hicho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya abiria walisema kuwa hali ya kituo hicho cha mabasi ni mbaya kwani katikati ya kituo kuna mifereji ambayo imekuwa ikipitisha maji wakati mvua na maeneo mengine kuna madimbwi yaliyojaa maji ambapo magari yanapita kwa taabu

Kuruthum Athuman mkazi wa kijiji cha mtwara pachani wilayani namtumbo ameuomba uongozi wa halmashauri hiyo kuona umuhimu wa kuchukua hatua za haraka za kukifanyia matengenezo kituo hicho ambacho kwa muda mrefu ni kibovu na kusababisha wakati mwingine magari kukwama katikati ya kituo hicho.

Adam Kumburu mkazi wa Ruhuwiko wilayani Mbinga ameeleza kuwa kutokana na ubovu wa kituo cha mabasi hasa kwa nyakati za masika abiria wamekuwa wakilazimishwa kupanda mabasi wakiwa nje ya kituo hicho kwa sabababu mvua zinapokuwa zinanyesha kituo hicho kimekuwa kikijaa tope jambo ambalo limekuwa likionekana kuwa ni kero kubwa kwa abiria.

Kwa upande wao baadhi ya wamiliki wa mabasi yanayotoa huduma ya kusafirisha abiria kutoka Songea kwenda Mbinga na kutoka Songea kwenda jijini Dar es Salaam wamesema kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwenye blog kuwa kituo cha mabasi cha mjini Songea ni kibovu sana na kina mashimo mengi ambayo husababisha magari yanayoingia na kutoka kwenye kituo hicho kutaka spiringi na kuwepo uharibifu wa mara kwa mara kwa baadhi ya vipuri vya magari yao. 

Walisema kuwa pamoja na kuwepo uharibifu wa magari yao na kutoa malalamiko ya mara kwa mara bado halmashauri inaendelea kukusanya ushuru wa kuegesha magari kwenye kituo hicho kila siku mfano magari madogo (taksi) hutozwa shilingi 500/= kwa siku moja, magari kuanzia tani tatu hadi tani kumi hutozwa kiasi cha shilingi 1000/= kwa siku kwa kila gari linaloegeshwa kituoni hapo na magari makubwa kuanzia tani kumi hadi tani kumi na tano linatozwa kiasi cha shilingi 2000/= kwa siku moja.
Walifafanua kuwa kwa wastani halmashauri ya manispaa hiyo imekuwa ikipata mapato makubwa kutokana na kuegesha magari kutoka katika kituo kikuu cha mabasi cha Songea kwani ni zaidi ya magari kati ya hamsini na sabini kwa siku yanaingia kituoni hapo na kutozwa ushuru wa maegesho. Hivyo wameumba uongozi wa halmashauri hiyo kuwa fedha zinazokusanywa kutokana na maegesho ndiyo zitumike kufanyia ukarabati wa kituo hicho ambacho ni kibovu kwa muda mrefu.

Walisema kuwa wameshangaa kuona zimeletwa kokoto tangu miezi miwili iliyopita na kurundikwa katikati ya kituo cha mabasi na mpaka sasa hakuna kinachoendelea na inaonekana kuwa kokoto hizo zimeletwa kwa kuhifadhiwa kwa muda na sio kwa ajili ya matengenezo ya kituo hicho kwani zingeletwa kwa matengenezo ya kituo hicho halmashauri ingekuwa imeshaanza kufanya kazi hiyo lakini kokoto hizo zimekuwa zikisababisha mabasi kuegeshwa kwa taabu.

Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Songea Nachoa Zakaria alipohojiwa ofisini kwake kuhusiana na tatizo la ubovu wa kituo cha mabasi cha mjini Songea alikiri kuwepo kwa tatizo hilo lakini aliwataka wakazi wa mjini songea pamoja na wamiliki wa mabasi kuwa watambue kuwa mara zote ujenzi mchakato hivyo kwa sasa wanatafuta vifaa  mbalimbali na wanaangalia uwezekano wa kupata lami kwani lengo kubwa la manispaa yake ni kukifanyia matengenezo kituo hicho kwa kiwango cha lami.

Alisema kuwa kokoto zilizomwagwa kwenye kituo hicho zimeletwa kwa msaada toka kampuni moja ya ujenzi wa barabara mkoani Ruvuma hivyo kwa sasa hivi halmashauri yake bado inashughulikia zabuni ya kumpata mtu wa kukijenga kituo hicho na amewataka kuwa wavumilivu na si vinginevyo.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO 17.04.2013



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Bungeni hakukaliki

Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla (kushoto), akiwasiliana na mwenzake wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga ndani ya Ukumbi wa Bunge Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi.
Baadhi ya wabunge jana waliendelea kutumia fursa ya mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu kurushiana vijembe na maneno ya kuudhi mambo ambayo yalisababisha mivutano ya kikanuni, huku mmoja wao akionya kwamba ikiwa haki hiyo itaendelea bungeni hakutakalika.

Chimbuko la mivutano hiyo ni kauli zilizotolewa na Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), Juma Nkamia ambaye alimjibu Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi kwamba “haongei na mbwa bali anazungumza na mwenye mbwa.”

Kadhalika Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde aliwapiga vijembe viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema kwamba kuna wabunge ambao wana “mimba zisizotarajiwa bungeni”.

Vijembe hivyo viliendelea jioni baada ya Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje kusema Serikali iliyopo madarakani haina uwezo, haina ujuzi na imepoteza imani ya watu kutokana na kushindwa kuwatatulia wananchi matatizo yaliyopo.


Naye Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa akieleza kuwa Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna “akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.”

Alitumia kifungu cha kitabu kitakatifu cha Biblia cha Mithali 27:22 kinachosema kuwa “mpumbavu ukimchukua ukimchanganya na ngano kwenye kinu atabaki na upumbavu wake.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Wenje na Msigwa walikiuka kanuni za Bunge kutokana na matamshi yao.

Naibu Spika, Ndugai alionya lugha hizo bungeni akiwasihi wabunge kuacha kutumia, kauli iliyoungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Anna Abdallah ambaye alieleza kukerwa na udhalilishaji wa wanawake bungeni.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Paulina Gekul akitumia Kanuni ya 68 (7) alikilaumu kiti cha Spika kwa kukaa kimya wakati wabunge wanatukana bungeni. “Kama hali hii itaendelea, humu ndani kutakuwa hakutawaliki,” alisema Gekul.

Pia Moses Machali (Kasulu Mjini -NCCR-Mageuzi) na Magdalena Sakaya (Viti Maalumu-CUF) waliomba mwongozo wa Spika wakitumia Kanuni ya 64 inayozuia lugha za kuudhi bungeni.


Lusinde alianza kuipiga vijembe hotuba ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na baadaye alidai kwamba wapo wabunge wenye mimba zisizotarajiwa ambao wanaharibu nchi.

“Ukiangalia kuna watu wanataka kuvuruga nchi wakati wana watoto wachanga. Mimi mtoto wangu wa mwisho ana miaka minane halafu Slaa (Dk Willibrod, Katibu Mkuu Chadema) wa kwake sijui ana wiki ngapi,” alisema Lusinde na kuongeza: “Hawa wapinzani tuachieni mimi na Mwigulu (Nchemba, Naibu Katibu Mkuu CCM).”

Baada ya Lusinde kumaliza Sakaya aliomba mwongozo wa Spika kuhusu utaratibu akitumia Kanuni ya 64(1) (g) , akisema kauli yake kwamba kuna wabunge ambao ni viongozi wana mimba zisizotarajiwa ni ya kuudhi.

Chanzo: Mwananchi

TAMKO LA CHADEMA KWA VYOMBO VYA HABARI


Ndugu waandishi wa habari;
LEO tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu, nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo mengi mno.

Uchunguzi huu nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.

Nimefanya hivyo kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.

Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.

Aidha, Nchemba amedai kumiliki video ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?

Kwamba genge hili la kina Nchemba na wenzake, walipanga kumteka Kibanda, wakatimiza lengo lao hilo, baadaye wakaingia kwenye plani B ya kutaka kuihusisha Chadema. Wakamtumia Ludovick Joseph Rwezahula ambaye ni mshitakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatare, kufanikisha mkakati wao huu wa kishetani.

Ndugu waandishi wa habari;
Huu ni mchezo mchafu na wahatari mno ambao kwa vyovyote vile, haupaswi kuvumiliwa. Kuanzia sasa nimeamua kwa dhati kabisa, kukomesha mchezo huu ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.

Kwa kuanzia, kesho Jumatatu, nitaongoza jopo la mawakili sita wa Chadema kumtetea Bw. Lwakatare. Wenzangu wengine katika kesi hii, ni Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu, Edson Mbogoro, Peter Kibatara na Nyaronyo Kicheere. Huko mbele tutaongeza mawakili wengine, akiwamo mmoja anayewekwa na familia ya Lwakatare.

Ndugu waandishi wa habari;
Mnaweza kujiuliza, kwa nini Chadema kimechukua uamuzi huu wa kuweka kundi kubwa la wanasheria katika kesi hii ya Lwakatare? Jibu ni kwamba tumegundua kuwa kesi hii imefunguliwa kwa lengo maalum la kuidhoofisha Chadema na kuinusuru CCM ambayo inakabiliwa na dhahama ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushamiri kwa makundi.

Hivyo wameamfungulia kesi Lwakatare, kwa lengo la kutaka kuaminisha umma kuwa Chadema ni chama cha magaidi, kinapanga ugaidi na hivyo kichukiwe. Hilo ndilo lengo lao. Basi!

Ndugu waandishi wa habari;

Pili, nitakwenda mahakamani kuwasilisha ombi maalum la kuomba amri ya mahakama kuagiza makampuni ya simu za mkononi kuwasilisha mahakamani statement za simu za watu kumi (10) ili kusaidia mahakama kutenda haki na jamii kujua ukweli wa mambo haya.

Watu ambao nitaomba mahakama itoe amri ya kuletwa taarifa zao simu
na meseji (sms) ni Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini (TISS), Jack Zoka, anayetumia simu Na. 255756809535, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Lameck Nchemba, anayetumia simu tano zikiwamo 0754 008888, 0757 946223, 0714 008888 na 0787 513446 na Ludovick Joseph Rwezahula, ambaye simu zake ni,0715 927100 na 0753 927 100.

Mwingine ambaye mawasiliano yake yanahitajika, ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, anayetumia simu Na. 0754 003388, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Mwananchi, Dennis Msaky anayetumia simu mbili, 0655 331010 na 0764 331010 na Bw. Sinbad Mwagha, ambaye ni afisa wa idara ya usalama wa taifa, anayetumia simu 0754 006355.

Wengine, ni Bw. Shaali Ali, afisa mwinge wa usalama wa taifa anayetumia simu Na. 0716990099, Saumu K. Malungu, mwenye kutumia simu 0719 541 434 na 0789 614 629, simu mbili zinazotumiwa na mtuhumiwa mkuu wa utekaji wa Dk. Steven Ulimboka, Bw. Ramadhani Abeid Igondo ikiwamo 0713 760 473, simu za Bw. Ridhiwani Kikwete ambazo ni 0754 566299, 0784 566 299, simu ya Dr. Steven Ulimboka, ambayo ni 0713 0713 731 610, pamoja na simu zote tatu za Willifred Lwakatare, ambazo ni 0786 774697, 0713 237869 na 0758 417169.

Ndugu waandishi wa habari;
Mtu mwingine muhimu nitakayeomba mahakama itoe amri ya kutolewa kwa taarifa zake, ni mwandishi wa habari na mpigapicha wa magazeti ya serikali, Muhidini Issa Michuzi. Mwandani huyu wa Ikulu, ndiye aliyeandika ujumbe kwa njia ya emeili kuipongeza ofisi binafsi ya rais (OBR) na usalama wa taifa kwa kupata video ya Lwakatare.

Pongezi za Michuzi kwa TISS ndizo zinanisukuma kuiomba mahakama kuagiza kupatikana taarifa zake. Michuzi anaipongeza TISS kwa kuibua njama za wahalifu, lakini mimi ninajua TISS ikipata njama za aina hiyo haraka inapeleka ushahidi polisi, lakini huu wa Lwakatare ulipelekwa Youtube, badala ya kwenye vyombo vya sheria.


Maneno ya Michuzi kwamba ni TISS imeibua hiyo video yanathibitisha ushiriki wa TISS kwenye mchezo huo mchafu, na kwamba Chadema kinajua kuwa Michuzi alishirikiana na watu wa usalama wa taifa katika kazi hiyo chafu. Software za video (editing) walizotumia zilitoka kwake. Fedha ya kuandaa hiyo video zilitoka usalama na Ikulu. Tunajua kuwa wale vijana wa Ada Estate na yule jamaa anayempelekea kigogo wa Jamii Forum, walilalamika sana kwa mmoja wa wamiliki wa JF.


Ndugu waandishi wa habari;

Chadema kinajua kuwa mmoja wa watuhumiwa hawa, Mwigulu Nchemba anafanya mipango na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom ili kumsaidia kufuta taarifa zake. Nachukua nafasi hii, kuionya kampuni hiyo kuacha kucheza mchezo huo kwa kuwa ni kinyume cha sheria za mamlaka ya mawasiliano (TCRA).

Tunahitaji mawasiliano haya kwa kuwa Mwigulu – zinaonyesha mtuhumiwa huyo akifanya mawasiliano mfululizo na Ludovick, yakiwamo yale ya tarehe 4 Machi 2013. Hii ilikuwa siku moja kabla ya Kibanda kutekwa.


Ndugu waandishi wa habari;

Hawa niliowataja ni watu muhimu sana katika upangaji wa mkakati wa utengenezaji wa video ya Lwakatare na vitendo vya kihalifu vya utekwaji wa Kibanda na tukio la kutekwa na kisha kutupwa msutuni kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini, Dr. Steven Ulimboka.

Kwa mfano, simu ya Mwigullu Nchemba, namba 0714 008888, 0756 008888 na 0757 946223, zimefanya mawasiliano mara kadhaa na Ludovick Joseph, Saumu K. Malungu, Jack Zoka, Ali Shaali na Ramadhani Ighondo. Mawasiliano hayo yalifanyika katika kipindi ambacho mgomo wa madaktari ulishamiri; baadaye yakarudi tena kati ya 26 Desemba mwaka jana na 15 Machi mwaka huu.


Miongoni mwa mawasiliano ambayo tunaona yanahusika na ujambazi huu, ni yale ya 28 Desemba, siku ambayo mkanda wa Lwakatare umerekodiwa; tarehe 4 hadi 6 Machi 2013, siku moja kabla ya Kibanda kutekwa na yale ya usiku wa manane (saa 8:17) wa 13 Machi 2013, ambako mchana uliofuata Lwakatare alikamatwa.

Huyu Mwagha ndiye aliyekuwa anatumika kuwasiliana na Saumu Malungu, ambaye tulimtaja kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kazi na Mwigulu na usalama wa taifa, kurubuni vijana wetu kwa fedha ili kutoa ushahidi wa uongo juu ya video ya Lwakatare.

Vilevile, mawasiliano ya Mwiguluna Mwagha, katika kipindi hicho nayo tunayahitaji. Kwa sababu, huyu Mwagha anayetumia simu 0754006355, mbali na kuwasiliana na Mwigulu, ndiye aliyekuwa anawasiliana na mmoja wa waliomteka Ulimboka; na ndiye aliyewasiliana na Saumu kati ya 20Januari na Machi 6 mwaka huu.

Ndugu waandishi wa habari;
Ludovick alifanya mawasiliano ya mwisho na Joyece Agustine, ambaye anatumia simu Na. 0717 559210, mawasiliano ambayo yalifanyika saa 5:13 usiku. Hiyo ndiyo ilikuwa simu yake ya mwisho usiku huo; katika siku hiyo Ludovick aliwasilisna na Joyce mara tisa kuanzia saa 12: 54 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mtandao wa Jamii Forum, ambako video ya Lwakatare ilitumwa, Ludovick alikamatwa Machi 15 mwaka huu. Hata hivyo, rekodi katika simu yake Na. 0715 927100 inaoyesha 17 Machi Ludovick alifanya mawasiliano na Joyce Augustino. Mawasiliano hayo yalifanyika saa 8: 9 usiku, wakati inadaiwa na polisi alishakamatwa.

Naye mhariri wa Mwananchi, Bw. Msaky ambaye anatajwa kutaka kutekwa na Ludovick na Lwakatare, amekuwa na mawasiliano kadhaa na Ludovick – mtu anayepanga kumteka. Ludovick na Msaky walifanya mawasiliano mfululizo kati 27 Desema 2012, siku moja kabla ya video ya Lwakatare haijarekodiwa na 7 Machi siku moja baada ya Kibanda kutekwa.

Msacky alitumia simu zake hizo mbili (0764 331010 na 0655 331010) kuwasiliana na Ludovick, huku Ludovick akitumia 0753927100. Mawasiliano ya 31 Desemba yalifanyika Ludovick akiwa Tegeta, jijini Dar es Salaam. Mawakala hawa wawili wa usalama wa taifa (Ludovick na Msaky), walikutana 31 Desemba 2012, katika hoteli ya Tamal, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Ndugu waandishi wa habari;
Baada ya kupitia taarifa hizi za mawasiliano ya simu za Mwigulu Nchemba, Ludovick Joseph, Ramadhani Ighondo na Saumu Malungu tumegundua yafuatayo: Kwamba, Ramadhani Ighondo, amefanya mawasiliano mara nyingi na Mwigulu, Mwagha na Zoka; naye Mwagha amefanya mawasiliano na Mwigulu na Saumu; naye Saumu amefanya mawasiliano na Mwagha, Mwiguluna Shaali Ali, ambaye ni afisa usalama wa taifa.

Tumegundua vilevile, kuwapo mawasiliano kadhaa kati ya Ludovick na Msaky; Ludovick na Mwigulu; Msaky na Nchimbi; Msaki na Mwagha, Samu na Mwagha na Ramadhani Ighondo Abeid, anayetuhumiwa kumteka Dk. Ulimboka na Mwanga na Mwigullu.

Tumegundua pia kuwapo mawasiliano kati ya Ulimboka na Ramadhani; Zoka na Ighondo na Ridhiwani na Ighondo. Mawasiliano haya yalifanywa mfululizo usiku wa Juni 2012 siku ambayo Dk. Ulimboka alitekwa.

Tumepata kufahamu pia kwamba baadhi ya watu waliotajwa na gazeti la MwanaHALISI kuwa waliwasiliana na Ighondo usiku wa Juni 26, mwaka 2012, wamefanya mawasiliano pia na Mwigulu, Mwagha na Shaali Ali.

Ndugu waandishi wa habari;
Mwagha ni afisa usalama wa taifa anayefanyakazi makao makuu ya idara hiyo. Ndiye yule anayetumika kuendesha michezo ya kuhonga wanasiasa wa CCM na upinzani. Ni Mwagha anayepanga wabunge na kuwapanga waongee nini kwa maslahi ya CCM. Ushenzi wote anaoongea Mwighulu bungeni, hupewa na Mwagha kwa maelekezo ya Jack Zoka.

Naye Shaali ndiye aliyekutana na afisa wetu wa usalama, Ahmed Sabula na mwenzake, Machi 29 mwaka huu katika hoteli ya See Cliff jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo kati ya Sabula, kijana wetu wa usalama na afisa usalama wa serikali Bw. Shaali alitaka Sabula akubali kutumika kwa kutoa taarifa za vikao vya chama, kuwasilisha kwake nyaraka za kamati kuu na kueleza mipango ya chama katika kesi ya Lwakatare.

Kwenye mpango huu, afisa huyo wa usalama wa taifa ambaye ninamfahamu vizuri, alimuahidi Sabula kiasi cha Sh. milioni 30 na kwamba fedha hizo angelipwa wiki iliyopita. Aliahidiwa pia kwamba kila nyaraka atakayopeleka atalipwa ujira.

Aidha, Sabula aliahidiwa kulipwa shilingi 500,000 (laki tano) kila mwezi; afisa wetu huyu ameripoti tukio hilo kwa viongozi wake wa chama. Yule mwenzake aliandaliwa kuwa shahidi wa kesi ya Lwakatare; aliambiwa akikubali dili hiyo atalipwa kila mwezi Sh. 500, lakini akaombwa kuwa mvumilivu kwa kuwa atalazimika kupotea kwa miezi kama mitano hadi sita.

Ndugu waandishi wa habari;
Kitendo cha Mwigulu kuwasiliana Ramadhani Ighondo, Mwigulu kuwasiliana na Ludovick, Saumu kuwasiliana na Mwigulu, Ighondo kuwasiliana na Ulimboka, Zoka kuwasiliana na Ighondo, tena katika muda uleule ambao Ighondo amewasiliana na Ulimboka na Saumu kuwasiliana na Mwagha, ni uthibitisho tosha kwamba usalama wa taifa wako nyuma ya mipango hii ya michafu ya kupanga utekaji na kisha kutaka kukichafua Chadema.

Aidha, kitendo cha Ludovick kuwasiliana Msaky; Ighondo kuwasiliana na Mwagha, Ridhiwani Kikwete kuwasiliana na Ighondo, tena kila baada ya Ighondo kuwasiliana na Ulimboka na Jack Zoka, ni uthibitisho mwingine kuwa genge hili la wahalifu linashirkiana na baadhi ya watu kutaka kuangamiza taifa.

Ni uthibitisho tosha kwamba hawa ndiyo wanaowahonga wanachama wa Chadema na watu wengine ili watoe ushahidi feki dhidi ya Lwakatare, na kwamba ni usalama wa taifa walioandaa ile video uchwara inayopigiwa chapuo na Mwigulu.

Ndugu waandishi wa habari;

Chama Cha Mapinduzi kinajua kwa hali ya sasa hakiwezi kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 huku Chadema ikiwa katika hali nzuri ya kisiasa tunayoiona sasa. Wanajua kabisa CCM imegawanyika, kundi lolote litakalopita ndani ya CCM, litahujumu kundi jingine. Ni kama ilivyotokea uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.

Ndiyo maana wanapanga kila mbinu kutaka kuiangamiza Chadema. Nasi tunasema katu hatutakubali kuona Chadema kinakufa. Tutapambana usiku na mchana. Juna na mvua. Hadi tushinde hila hizi.Tunawaambia wanachama wetu na wale wanaotuunga mkono, Chadema ni chama kikubwa. Kina mtandao kila mahali, kuanzia Ikulu hadi polisi; na hivyo hakitakufa au kuzorota kwa mambo ya kupikwa.

Ni imani yangu kwamba amri ya mahakama itawafichua wote hawa ni kuirudisha Tanzania katika amani yake. Ni lazima tufikike mahala watu hawa wafahamike mbele ya umma, tunataka wafahamu kuwa maisha ya mwanadamu yana thamani kuliko siasa chafu na ufisadi wanaouendeleza.

Nawashukuru kwa kunisikiliza.


Mabere Marando,

Dar es Salaam

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI 14.04.2013

ALIYEFARIKI 2008 NA KUZIKWA AONEKANA JANA AKIWA HAI KATIKA MAZINGIRA TATA..SOMA RIPOTI KAMILI HAPA

mwanamke anayedaiwa kufariki miaka mitano iliyopita 
Kwa ufupi
Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.

Geita: Mji wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa.
Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.
Aliyekuwa wa kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada yake.
“Baada ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada (Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia anafanana na marehemu dada yetu,”alisema Jubili na kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka nje.
Alisema mtoto wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali ya Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.
Rebeka ambaye ni mtoto wa nne wa Flora alisema: “Mama mdogo alituita sisi tulikuwa tumelala akasema kwamba nje kuna mwanamke ambaye anafanana na marehemu mama yetu, ndipo na sisi tukatoka na kweli kumwangalia alikuwa ni yeye kabisa.”
Alisema walipomuhoji mama yake huyo kwamba ametokea wapi, aliwaeleza kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga na aliletwa na watu ambao hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya gari na watu hao walimshusha kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni jirani na dada zake hao.
Kauli ya Flora
Akizungumza na waandishi wa habari, Flora alisema yeye ni mkazi wa Katoro na kwamba alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi ambaye hata hivyo hakumtaja kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini) wamemkataza.
“Nilikuwa naishi kwa mganga wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati nikiwa pale akaninywesha dawa kisha tukapakizwa kwenye gari na watu wawili ambao sikuwatambua, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume mpaka hapa Kasamwa tukashushwa saa 1:00 jioni,”alisema Flora.
Alisema alipofika Kasamwa alikwenda kunywa uji kwa mama mmoja ambaye pia hakumtaja na kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine saa nne usiku, lakini watu wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia: “Hapa si kwako twende tukupeleke kwa ndugu yako” na ndipo wakampeleka kwa dada yake ambako aliketi nje hadi alfajiri.
Flora alisema kabla ya kuishi kwa mganga alikuwa akiishi porini ambako alitupwa na watu asiowafahamu na baadaye aliokotwa na wasamaria wema ambao ndiyo walimpeleka kwa mganga ambako alikuwa akiishi muda wote.
Kuhusu ndugu, Flora alisema ana ndugu zake Sengerema na Geita kwamba Sengerema ndiko alikokuwa akiishi kabla ya kwenda porini.
Kadhalika mwanamke huyo anayedaiwa kufufuka alisema ana watoto watano, (idadi ambayo ni sawa na ile aliyoacha marehemu Flora), lakini alipoambiwa awataje alikuwa akichanganya majina.
Ndugu wapishana
Baba mzazi wa mwanamke huyo, James Tunge ambaye aliitwa baada ya kutokea tukio hilo alisema kuwa mwanaye alifariki, lakini anashangaa kuona leo anaonekana tena.
Hata hivyo, Tunge alisema alipomwona mwanamke huyo juzi asubuhi alikuwa akifanana kabisa na mwanaye Flora, lakini alipoondoka kwenda kufuata picha yake na kurejea alikuta amebadilika, kwani kovu alilokuwa nalo kabla ya kifo halikuwa likionekana.
“Kwa sasa naweza kusema huyu siyo ila asubuhi wakati namwona ni kweli alikuwa mwanangu marehemu, najua mwanangu alikuwa na kovu kubwa puani na shavu la kushoto, lakini sasa hivi anaonekana ana kovu moja la shavuni ila sehemu zingine za mwili wanafanana kabisa,”alisema Tunge.
Kwa upande wake Jubili alisema kuna kila dalili kwamba mwanamke huyo ni mdogo wake, kwani anavyojieleza maelezo yake yanafanana. Alisema anawatambua watoto wake na ndugu japo wakati mwingine ni kama anapoteza kumbukumbu na kubadilika badilika sura.
“Wakati tunamwona asubuhi alikuwa akifanana na dada yangu marehemu, kwani dada alikuwa na kovu kubwa puani na shavuni na kweli alikuwa nalo na baadaye tulipoendelea kumuhoji alianza kubadilika sura na mara kovu likawa halionekani tena, “alisema Jubili.
Kwa ujumla ndugu wa mwanamke huyo wanahusisha tukio hilo na ushirikina kwa kusema kwamba huenda ndugu yao alichukuliwa kwa njia za giza, lakini Mungu amemwezesha kurejea katika maisha ya kawaida.
Jubili alisema kifo cha Flora miaka mitano iliyopita kilikuwa cha mazingira ya kutatanisha, kwani aliugua ghafla baada ya kula viazi vitamu kwenye mji wa jirani na hapo kuanza kuvimba tumbo.
Kwa kuzingatia mazingira hayo, juzi Flora alipelekwa wilayani Sengerema kwa mganga wa jadi aliyejitambulisha kwa jina la Dk. Mkonogi Masendena .
Kabla ya kupelekwa Sengerema, suala hilo lilifikishwa polisi ambao baadaye waliruhusu Flora kuondoka na wanaodai kwamba ni ndugu yao na hata walipofika Sengerema walilazimika kwenda polisi kwanza.
Polisi mkoani Geita walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba ndugu zake waliondoka naye.
Mwananchi

NAFASI MPYA ZA KAZI "WOLD VISION TANZANIA"......CHANGAMKIA ..MWISHO JUMATATU

World Vision is urgently recruiting qualified Tanzanian citizens to fill the below positions:

1:Security Adviser


2:Senior Internal Auditor


3:Internal Auditor


4:External relations Manager


5:
Sustainable Local Institutions Coordinator

6:Sr.Program Officer


For details on job descriptions and how to apply visit our blog at:
WORLD VISION TANZANIA CAREERS

NOTE:World Vision Tanzania does not charge any fees or ask for any payment in any stage of recruitment.DO NOT accept any request of payment.We only use e-mail dresses with a domain name wvi.org and not any other e-mail domain names such as yahoo,hotmail etc.

BAADHI YA WABUNGE WAMEENDELEA KUJADILI KESI INAYOMKABILI WILFRED LWAKATARE LICHA YA KESI HIYO KUWA MAHAKAMANI

makinda
Bila kujali kwamba kesi ya Ugaidi na kula njama ya kutenda kosa la jinai inayomkabili Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), WILFRED LWAKATARE na mwenzake LUDOVICK RWEZAURA kuwa mahakamani, baadhi ya Wabunge wameendelea kulijadili suala hilo na kubainisha mkakati huo ulivyopangwa.

MWIGULU NCHEMBA Mbunge wa Iramba Magharibi ndiye aliyefungua pazia la malumbano hayo akidai kujibu Hotuba ya Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayomtaka akamatwe kwa ugaidi na kusema anao ushahidi wa kutosha na yuko tayari kwenda popote kuthibitisha jambo hilo.

Kambi ya Upinzani ikiwakilishwa na Mbunge wa Mbulu MUSTAPHA AKUNAI inaoneshwa kuchukizwa na kauli hiyo na kupelekea kuomba muongozo wa Spika ili hoja hiyo isijadiliwe Bungeni.

Hata hivyo kwa kutoridhishwa na kauli hiyo ya kiti cha Spika, Mbunge wa Singida Mashariki TUNDU LISSU anairudisha tena hoja hiyo iliyopo mahakamani kwa madai kwamba mkakati mzima umepangwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara MWIGULU NCHEMBA.

Baadae Mbunge wa Viti Maalum ANNA ABDALAH nae akaingilia kati na kuomba muongozo hali inayompelekea Spika MAKINDA kuwataka wabunge kuachana na jambo hilo ili wajadili masula yanayowahusu wananchi kwa ujumla.

Mbali na hayo bunge limeendelea na majadiliano ya Makadirio na Matumizi ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Matumizi ya Bunge na kuahirishwa hadi Juni 15 saa tatu asubuhi mwaka huu.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TEREHE 13/04/2013

.....
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC04369
.
DSC04370
.
DSC04371
.
DSC04372
.
DSC04373
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top