Kamishna wa polisi ambaye ni mkuu wa operation wa jeshi la polisi, amezungumza na waandishi wa habari mjini hapa na ameelezea tukio zima ambapo amekanusha uvumi uliopo kuwa kuna mauaji kadhaa ya kishirikina yametokea mjini Songea, lakini amebainisha kuwa kumetokea wimbi la mauaji ambapo zaidi ya watu 14 wameauawa katika matukio tofauti, tangu novemba mwaka jana hadi sasa na hakuna hata mtu mmoja aliyeuawa kwa ushirikina. Kwani kila tukio la mauaji lilifanyiwa uchunguzi yakinifu kwa kushirikaina na viongozi wa serikali na polisi lakini hakukuwa na upungufu wa aina yoyote ya viungo katika maiti hizo.
Kutokana na hali hiyo wananchi wengi walipitisha uvumi kuwa ni lazima ifanyike fujo ili kulishinikiza jeshi la polisi lifanye kazi wakiamini kwamba matukio hayo yalikuwa na ya kishirikina.
Amewataka wananchi waache tabia ya kuchukua sheria mikononi kwani kufanya hivyo ni kuvunja amani iliyopo, hasa ikizingatiwa mkoa wa Ruvuma husasani Songea ni mji wa amani.
Mwishoni alimalizia kwa kusema amani haiji kwa ncha ya upanga.
Post a Comment