Akihojiwa na radio moja inayorusha matangazo yake hapa Songea kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi la polisi hapa mkoani alisema maandamano yaliyofanyika jana hapa mjini yameshinikizwa na vyama vya siasa na wanaharakati. Huku akishindwa kusema ni chama gani kilichoshinikiza maandamano hayo ambayo yeye anayaita vurugu. Aliongeza kusema kuwa wanasiasa na wanaharakati hao waliwahonga watu pesa ili waandamane. Alipoulizwa anauhakika gani na hilo akasema hizo ni taarifa za kiinterejensi.
Alipoulizwa kuhusu polisi kutumia nguvu zaidi katika kupambana na waandamanaji yeye alisema inapobidi nguvu lazima zitumike, lakini itaundwa tume ya kuchunguza mauaji hayo.
MAONI KUHUSU HALI HII.
- Kila mtu anaweza kujiuliza inawezekanaje chama au wanaharakati kuwapa pesa mamia ya raia ili waandamane na kila raia alipewa shilingi ngapi?
- Je inawekanaje wanaharakati na wanasiasa wakawa wanauchungu zaidi kuliko watu waliofiwa?
- Kuhusu askari kutumia nguvu mimi nilikuwepo eneo la tukio na risasi moja ilipiga hatua chache toka nilipokuwa na mita chache mbele ilimuua mtu mbele ya macho yangu. Ukweli ni kwamba nguvu iliyotumika ilikuwa kubwa sana, kwani polisi (FFU) walipofika hawakutoa tangazo lolote la kuwataka raia watawanyike bali walianza kurusha risasi za moto na mabomu ya machozi na kupelekea maafa.
RAIA
Raia wakati wa maandamano hayo ni kweli walikuwa wanarusha mawe hasa katika maeneo ya kwa mkuuwa mkoa na pia nilishuhudia raia wakiwafukuza askari polisi kwa mawe, askari hao walikuwa karibu na maandamano hayo.
LAKINI JE HAYO YOTE YALIYOTOKEA YALISTAHILI?
Post a Comment