Na Julius Konala,Songea
WATOTO wote watano waliozaliwa juzi katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wamefariki usiku wa kuamkia jana .
Watoto hao wote watano walizaliwa salama na Sophia Mgaya (28)
mkazi wa Ruhuwiko mjini hapa kwa
kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya
mkoa wa Ruvuma.
Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Songea(HOMSO)Dkt.
Benedict Ngaiza, alisema kuwa watoto hao wameishi kwa masaa kumi tu na kufariki
dunia kutokana na kuzaliwa na uzito
mdogo wa chini ya kilo moja.
Dkt.Ngaiza alibainisha
kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo wanakuwa na maisha
mafupi,hata hivyo alisema hali ya mama wa watoto hao inaendelea vizuri ingawa
bado amelezwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiendelea kupata matibabu.
Tukio ambalo halijawahi kutokea katika hospitali ya mkoa wa
Ruvuma limetokea Mei 24 mwaka huu majira
ya saa 4 asubuhi huku mtoto wa kwanza
akiwa na uzito wa gramu 730,wa pili 810,watatu 670,wanne 820 na watano gramu
430.
Kulingana na mganga huyo kati ya watoto hao waliozaliwa,watatu
ni wa kiume na wawili ni wa kike na
kwamba huu ulikuwa ni mzao wa pili kwa mwanamke huyo.
Alieleza kuwa katika mzao wa kwanza wa mama huyo alifanikiwa
kujifungua mtoto mmoja na huu wa pili amebahatika
kujifungua watoto hao watano ambao wote wamefariki dunia .
Post a Comment