Loading...

CHADEMA, CCM wahitimisha kampeni kwa kishido Songea.

Na songeayetu.blogspot.com

Vyama viwili vya siasa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa pamoja vimeweza kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani unaotarajia kufanyika kesho tarehe mosi Aprili mwaka huu.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika kwa lengo la kuziba pengo la aliyekuwa diwani wa kata ya Lizaboni  mh.Manya aliyefari na kuachwa wazi kwa nafasi hiyo. Katika hali ya kutetea kwa nafasi ya kiti hicho chama cha mapinduzi katika ufungaji wa kampeni hizo uliofanyika katika viwanja vya sokoni maeneo ya Lizaboni stendi wameapa kurejesha kiti hicho kutokana na umakini wao katika siasa pamoja na kujipanga sawa sawa katika kuitetea nafasi hiyo.
 Kwa upande wa meneja kampeni wa chama hicho amesema kuwa CCM ni chama imara na chenye mipango imara kwani aliweza kuwatuhumu baadhi ya wapinzani ambao waliweza kumkashifu mgombea wao kuwa ni bubu, na kudai mbele za wapiga kura kupuuzia madai hayo na kumnadi mgombea wake kuwa ni kiongozi bora na ambaye anautashi mkubwa katika uongozi na kumtupia kijembe mgombea wa CHADEMA, ndugu Nilongo kuwa ni muongo ambaye hawezi kutekeleza ahadi zake na kuhusisha jina nilongo na muongo katika moja wapo ya lugha za kibantu.  
Baada ya kuhitimisha kampeni hizo, gari aina ya Toyota, ambalo lilikuwa likiwasambaza baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi lilipata ajali muda mfupi mara baada ya kampeni kwa kumshinda derive kulimudu na kugonga mti na kupinduka katika barabara iendayo kituo cha afya cha mji Mwema mita chache kutoka nyumbani kwa aliyekuwa diwani wa kata hiyo Marehemu Manya.
Nacho chama cha demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) kwa upande wake kiliweza kuhitimisha kampeni zake katika viwanja vya shule ya msingi Kiburang’oma, kwa upande wake waliweza kujihami na kuhakikisha kutwaa kiti hicho cha udiwani kwa kuhusisha na historia ya uchaguzi mdogo katika manispaa ya Songea. Ikumbukwe kuwa CHADEMA waliweza kutwaa kiti cha udiwani katika uchaguzi mdogo kwa kata ya Majengo hivyo na kuamini kutumia wembe uleule waliotumia kupata kata ya Lizaboni.
Naye Mh. Chiku Abwao, (CHADEMA) mbunge wa viti maalum katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye ameongoza kampeni katika kata hiyo katika ufungaji wa kampeni za chama chao, alidai kuwa upande wao wamejipanga kikamilifu kutwaa kata hiyo mikononi mwa chama chao. Chiku alisisitiza zaidi amani kuwa Chadema inahitaji kuona amani inatawala katika manispaa ya Songea kwa kusisitiza kuwepo kwa uchaguzi wa amani na haki hapo kesho. Iwapo kanuni na sheria za uchaguzi zitakuwa zikigeuzwa basi nguvu ya umma ndiyo itakayoamua, kwani aliwasisitiza vijana kulinda kura zao kwa kupiga kura na kukaa mita mia mbili maeneo yote ya vituo vya uchaguzi.
Kwa upande wa mgombea udiwani CHADEMA kwa nafasi yake ya mwisho katika kuhitimisha kampeni aliashukuru wananchi wote waliojitokeza kuanzia siku ya kwanza hadi ufungaji wa kampeni. Aliweza kuahidi kushughulikia matatizo ya wananchi wake wote bila kujali itikadi kuanzia watoto, vijana na wazee pamoja na makundi mengine kama vile walemavu, wagonjwa wa akili, wavuta bangi wote kwa pamoja atawasaidia kwani kwa pamoja ni wananchi wake wote. Hivyo aliahidi kuondoa kero za michango kwa wananchi wake kwani kuna fedha zipo zimetolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ambapo zinatakiwa zitumike kwanza, zikiisha ndipo wananchi wachangishwe fedha za maendeleo na kuapa kulisimamia suala hilo mapema kuanzia jumanne baada ya uchaguzi wa kesho jumapili.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top