Na Gideon Mwakanosya
Mfanyabiashara mmoja anayejishughulisha na ukandarasi katika halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Joseph Mrema (31) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoni humo akikabiriwa na shitaka la kumjeruhi askari polisi mwenye namba E 9507 PC Lucas Komba wa kituo kikuu cha polisi Tabora kwa kupiga risasi kwa kutumia silaha aina ya bastora kwenye mapaja ya kushoto na kulia.
Katika mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Ruvuma Frank Mahimbali, mwendesha mashtaka alidai mahakamani hapo kuwa Mei 20 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku huko katika eneo la Seedfarm lililopo ndani ya manispaa ya Songea isivyohalali na kwa kukusudia alimjeruhi askari polisi PC Lucas Komba kwa kumfyatulia risasi kwa kutumia silaha aina ya bastora anayomiliki kihalali kwenye mapaja ya kushoto na kulia nakumsababishia majeraha makubwa.
Upande wa mashtaka ambao uliongozwa na wakili wa serikali Shaibu Mwegola ulidai kwamba upepelezi kuhusiana na mshitakiwa Mrema bado haujakamilika hivyo aliiomba mahakama ione umuhimu wa kupangwa kesi hiyo.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kupata wadhamini wawili kwa dhamana ya sh. Milioni moja kila mmoja kwa masharti ya kuwa wahakikishe kuwa mshitakiwa Mrema anafika mahakamani bila kukosa mpaka kesi yake itakapokwisha na kesi hiyo imeahilishwa hadi June 18 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Post a Comment