Loading...

WAGONJWA WAKOSA HUDUMA YA X RAY HOSPITALI YA MKOA SONGEA

Na Gideon Mwakanosya
Baadhi ya wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Songea wameimba serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii kuona umuhimu wa kuifanyia matengenezo X-ray ya hospitali ya serikali ya mkoa wa Ruvuma ambayo imeshindwa kutoa hiyo kwa wagonjwa kwa muda mrefu na kusababisha wagonjwa wanaotakiwa kupata huduma hiyo kwenda kwenye hospitali ya Peramiho ambako ni mbali na Songea mjini.

Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa maeneo ya Mfaranyaki, Mjimwema, Ruhuwiko na Mshangano ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walieleza kuwa kwa muda mrefu sana huduma ya X ray katika hospitali ya mkoa haipatikani na wanapokwenda hospitalini hapo kupata huduma wamekuwa wakishauriwa kwenda Hospitali ya misheni ya Peramiho ambako ndiko huduma hiyo kwa sasa inatolewa.

Wananchi hao walisema kuwa ni vyema serikali ikaangalia uwezekano wa kuitengeneza mashine hiyo ambayo hapo awali ilikuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Songea na wagonjwa wanaotoka kwenye wilaya nyingine kama vile Mbinga, Natumbo, Tunduru na wilaya mpya ya Nyasa.

Walitoa mfano kuwa hivi karibuni katika eneo la Seedfarm kwenye barabara itokayo Songea kwenda Namtumbo gari la jeshi la wananchi liliwagonga watu wanne ambao walikuwa wakitembea kwa miguu na kusababisha watu wawili kufa papo hapo na wengine wawili walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya serikali ya mkoa ambako mmojakati yao baadae ililazimika kumpeleka Peramiho baada ya hospitali hiyo kukosa huduma ya X ray jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa Songea na maeneo mengine.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr Benedict Ngaiza alipohojiwa na NIPASHE kuhusiana na malalamiko hayo alikirikuwa mashine ya x ray ya hospitali ya serikali ya mkoa wa Ruvuma bado ni mbovu tangu mwezi mmoja uliopita.

Dr Ngaiza ambaye pia ni mganga mfawidhi wa hospitali ya serikali ya mkoa Songea alisema kuwa pamoja na kwamba katika hospitali yake haukuna huduma hiyo ya x ray lakini wagonjwa wanaohitajihuduma hiyo hushauriwa kwenda kupta huduma hiyo kwenye hospitali ya misheni ya Peramiho licha ya kuwa nayo maashine ya hospitali hiyo inaubovu haifanyi kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

Alisema kuwa changamoto baadhi ya huduma zinazohusisha huduma ya x ray katika hospitali ya mkoa zimesimamishwa kwa sasa. Hadi hapo wataalamu toka wizara ya afya na ustawi wa jamii watakapofika na kuja kuifanyia matengenezo.

Alieleza zaidi kuwa kwa mujibu wa taarifa toka wizara ya afya na ustawi wa jamii mafundi wanatarajiwa kusambazwa katika hospitali zote za serikali zenye mashine za x ray kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo x ray hizo ikiwemo na x ray ya hospitali ya serikali mkoa Songea.

Alifafanua zaidi kuwa pamoja na matengenezo yanayotarajiwa kufanyika bado hali si nzuri kwani chumba cha x ray kinatarajiwa kufanyiwa urakabati mkubwa ambao utafanywa kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu. Hivyo hata kama mashine hiyo itakapo tengenezwa bado huduma ya x ray itasimama hadi ukarabati wa chumba hicho utakapo kamilika.




Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top