Loading...

Polisi Ruvuma wawasaka majambazi waliotaka kumpora fedha mfanyabiashara


JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linalisaka kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha za moto ambao wanadaiwa kutaka kumpora fedha mfanyabiashara wa kijiji cha Unyoni wilayani Mbinga akiwa kwake ambao baadaye walikimbia na kutokomea kusikojulikana

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusidelit Msimeki alisema kuwa tukio hilo lilitokea juni 5 mwaka huu majira ya saa 2:45 usiku huko katika kijiji cha Unyoni ambako Satico Kapinga (42)ambaye anajishughulisha na biashara akiwa dukani kwake inadaiwa kuwa alivamiwa na kundi la watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha aina ya shortgun greener yenye namba 50340 

Alisema kuwa kundi hilo la watu lilikuwa na silaha ambayo ilikuwa imekatwa mtutu pamoja na kitako kwa lengo la kufanya unyang’anyi kwa mfanyabiashara huyo ambaye baada ya kuwaona watu hao ambao aliwahisi kuwa ni majambazi alianza kupiga kelele kwa ishara ya kuomba msaada kwa majirani na baadaye majambazi hao walikimbia na kutokomea kusikojulikana na silaha waliyokuwa nayo waliitelekeza baada ya kuona wamezidiwa nguvu na wananchi waliofika kwenye eneo hilo la tukio

Alieza zaidi kuwa majambazi hao wakiwa wanakimbia kwa kutawanyika wananchi wa kijiji hicho waliendelea kuwasaka bila kuwa na mafanikio ya aina yoyote na baadaye ndipo walipogundua kuwa silaha hiyo ilikuwa imetupa jirani na duka la Kapinga ambaye walitaka kumvamia na kumpora fedha alizokuwa nazo

Hata hivyo kamanda Msimeki alisema kuwa jeshi la polisi mkoani humo linafanya uchunguzi zaidi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini wale wote waliohusika na tayari jeshi lake limejipanga kikamilifu kukabiliana na majambazi



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top