TAREHE 5 mwezi wa sita ni sikuu ambayo duniani kote huadhimisha siku ya mazingira. Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mt. Agustino cha Tanzania, tawi la Songea wameweza kuadhimisha siku hiyo ya utunzaji mazingira kwa vitendo kwa kufanya usafi katika uwanja wa mpira wa Majimaji uliopo katika manispaa ya mji wa Songea.
Katika kutekeleza hilo, wanafunzi hao kwa idadi yao kubwa wameonekana wakihangaika kusafisha uwanja huo ambao kwa kiasi kikubwa unaonnekana kutelekezwa kwani kwa mtu ambaye ni mgeni anaweza kubaini kuwa uwanja huo hautumiwi kwa shughuli yoyote kutokana na kukuthiri kwa uchafu pamoja na kuwa na majani yasiyo na tija kuzunguka uwanja huo muhimu na tegemeo kwa mkoa wa Ruvuma.
Katika kuadhimisha sherehe hizo wanafunzi hao walionekana wakifanya usafi wakifurahia maadhimisho hayo kutokana na kujitoa na kufanya shughuli za usafi ambapo walikuwa wametegemea kuanza kufanya usafi katika maeneo ya soko la Manzese lililopo jirani kabisa na uwanja wa mpira wa miguu wa majimaji ambapo ndipo waliweza kuufanyia usafi kutokana na baadhi ya wafanya biashara wa soko la Manzese kutokuwa tayari kuwapa ushirikiano wanafunzi hao kufanya usafi katika maeneo yao kutokana na kudai kuwa muda huo walikuwa wanaendelea na shughuli zao za kibiashara.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa Majimaji wanafunzi hao waliweza kukutana na kikwazo kingine ambapo lango la kuingilia uwanjani hapo lilikuwa limefungwa kiasi cha wanfunzi hao kukaa nje ya uwanja huo takribani zaidi ya nusu saa huku wahusika wakitafutwa bila mafanikio. Baadaye wahusika walipopatikana ilionekana hawawakuwa na funguo za kufungulia milango ya uwanja huo ambapo waliweza kuamuru kuvunjwa kwa kufuli mojawapo katika malango ya uwanja huo.
Baadhi ya wanafunzi wameweza kuelezea kuwa zoezi hili la uhamasishaji wa usafishaji wa mazingira waliouonyesha katika manispaa hii ya Songea itakuwa endelevu kwa kufanya katika maeneo mbalimbali
Post a Comment