JESHI la polisi mkoani Ruvuma limewatia mbaroni wakazi wawili wa vijiji vya Menimtwalo na Mtina vya wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kukutwa wakiwa na vipande kumi na mbili vya nyama ya boko kwenye mbuga ya wanyama ya taifa ya Mwambesi wilayani humo
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Delisdelit Msimeki zilisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6.00 mchana huko katika hifadhi ya wanyama poli ya mbuga ya taifa ya Mwambesi
Kamanda Msimeki alisema kuwa siku hiyo ya tukio askari wa idara ya wanyama pori wakiwa kwenye shughuli zao za kazi za kila siku ghafla waliwaona watu wawili wakiwa wamebeba kifurushi ambacho kilizungushiwa kwenye mfuko wa kiroba
Alieleza zaidi kuwa askari hao wa wanyama pori baadaye walifanikiwa kuwakamata Halfani Said Halfani (45) mkazi wa kijiji cha Menemtwalo na Rashid Rusenge (32) mkazi wa kijij cha Mtina wakiwa na vipande kumi nambili vya nyama ya kiboko
Alisema kuwa watuhumiwa Halfani na Rusenge wanashikiliwa na polisi na wanendelea kuhojiwa zaidi na kwamba wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu upelelezi wa tukio hilo utakapo kamilika.
Post a Comment