JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu watatu wanaodaiwa kuwa ni wawindaji haramu ambao baada ya kukurupushwa kwenye pori la Mbalang’andu lililopo kwenye mbuga ya wanyama ya Selou wilayani Namtumbo na askari polisi wameitelekeza siraha aina ya riffle na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza ofisi kwake leo kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Delisdelit Msimeki alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku huko katika pori la Mbalang’andu lililopo katika kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo
Kamanda Msimeki alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio askari polisi wakiwa kwenye dolia walifanikiwa kukamata silaha aina ya riffle Winchester yenye namba 860155 model 70458 win magna ambayo inadaiwa kuwa ilikuwa ikitumiwa na wawindaji haramu kwenye pori la Mbarang’andu.
Alisema kuwa watuhumiwa watatu ambao baada ya kukurupushwa na polisi walikimbia na kuiterekeza silaha hiyo majina yao hayakuweza kufahamika mara moja licha ya kuwa taarifa za awali zilidai kuwa kulikuwa na kundi kubwa la wawindaji haramu kwenye eneo hilo ambao walikuwa wakiwinda wanyama bila kuwa na kibali kutoka idara ya wanyama pori.
Hata hivyo kamanda Msimeki alieza kuwa jeshi lake la polisi mkoani humo bado linaendelea kufanya upelelezi wa kina ili kuwabaini wawindaji haramu ambao waliiterekeza silaha baada ya kuvamiwa na polisi waliokuwa kwenye dolia kwenye pori hilo la Mbalang’andu na kwamba polisi inaendelea kuwasaka wawindaji haramu kwenye eneo la mbuga ya hifadhi ya wanyama ya taifa ya selou.
Post a Comment