Rais Jakaya Kikwete |
RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KESHO ANATARAJIWA KUZINDUA RASMI MATOKEO YA AWALI YA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI.
SHEREHE ZA UZINDUZI HUO UTAKAOAMBATANA NA KUTANGAZA KWA MATOKEO YA IDADI YA WATANZANIA ZITAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM NA ZITAHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA KITAIFA NA WANANCHI.
KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA AWALI YA IDADI YA WATU,NI HATU YA MWANZO KATIKA UTARATIBU WA UTOAJI WA TAKWIMU ZITOKANAZO NA SENSA YA WATU NA MAKAZI,AMBAPO MATOKEO MENGINE YATAENDELEA KUTOLEWA KWA AWAMU.
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU NA OFISI YA MTAKWIMU MKUU WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR, INAWATAKA WANANCHI,WANAHARAKATI NA WADAU WENGINE WOTE WA MAENDELEO KUTUMIA TAKWIMU HIZO KWA UFANISI WA MAHITAJI YAO NA MAENDELEO YA TAIFA KWA UJUMLA.
ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI LILIFANYIKA TANZANIA NZIMA KUANZIA TAREHE 26 AGOSTI HADI TAREHE 8 SEPTEMBA MWAKA HUU.
Post a Comment