Loading...

MBUNGE WA SONGEA MJINI AKABIDHI MAGARI MAWILI KWA WANANCHI WAKE



Na Nathan Mtega,Songea yetu

Mbunge wa jimbo la songea mjini mkoani Ruvuma  Leuindas Gama amekabidhi magari mawili kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa jimbo ilo ambayo ni gari kwa ajili ya kubeba wagonjwa na moja likiwa kwa ajilki ya kuwsaidia wananchi hao wa jimbo hilo wanapopatwa na matatizo ya msiba au kufiwa kama sehemu ya ahadi zake za kushirikiana na wananchi alizozitoa kwao wakati kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Maji maji wa mjini Songea wakati akikabidhi magari hayo amesema kwa kutambua changamoto za kipato na kiuchumi kwa wananchi walio wengi wa jimbo hilo la Songea zinazowakabili na kwa kuzingatia ushauri alioupata wakati wa kampeni hizo za uchaguzi na baada ya uchaguzi ameamua kuekeleza kwa vitendo ushauri huo.

Amesema magari hayo aliyokabidhi kwa wananchi yanapaswa kutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo huku akiongeza kuwa wasimamizi wakuu wa magari hayo ni wenyeviti wa mitaa wakishirikiana na katibu wake ambaye anawafahamu wenyeviti wote wa mitaa wa manispaa ya Songea na anaamini hakutakuwa na udanganyifu wala ubadhirifu katika matumizi ya magari hayo.

Wakizungumza baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye hafla hiyo mbali ya kupongeza na kushukuru kwa uamuzi huo wa mbunge wameahidi kuhakikisha magari hayo yanatunzwa na kutumiwa kwa madhumuini yaliyokusudiwa ambayo yanailenga jamii yote ya wananchi wa Manispaa hiyo ya Songea.

Aidha akizungumzia adha inayolalamikiwa na wananchi walio wengi ya kufungwa kwa kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea kwa ajili ya kupisha matengenezo ambayo yamechukua muda mrefu na kuanzishwa kwa kituo kipya cha mabasi kilichopo eneo la Msamala hali ambayo imekuwa ikiwagharimu wananchi kiasi kikubwa cha fedha wanapohitaji kusafiri Gama amesema matengenezo ya kituo hicho cha awali cha mabasi yamekamilika na baada ya wiki moja kituo hicho cha awali kitazinduliwa.

Amesema baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho cha mabasi cha awali mabasi yatakuwa na njia mbili tofauti kwa ajili ya kuingia na kutoka kwenye kituo hicho ili kuepusha usumbufu kwa watumiaji wa usafiri huo na kuongeza kuwa kituo kipya cha mabasi cha Msamala kitaendelea kutumika kwa mabasi hayo kupitia na kuendelea na safari za kwenda nje ya mkoa au kuingia kuelekea kituo kikuu cha mabasi cha awali.

MAJIMAJI SELEBUKA YAWA GUMZO TENA MJINI SONGEA 2016

MAJI MAJI SELEBUKA-Brochure2(1)

MAJIMAJI SELEBUKA YAWA GUMZO TENA MJINI SONGEA 2016

Maji maji Selebuka ni tamasha linaloandaliwa na kampuni binafsi iitwayo Tanzania Mwandi Co. Ltd ikishirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali liitwalo Songea-Mississippi (SO-MI). Shirika hili linahusika na mambo ya maendeleo ya jamii na elimu kwa wanaSongea kwa ushirikiano kati ya Songea Tanzania na Mississippi Marekani tangu lilipoanzishwa 2008.
Mwaka huu shirika limeandaa tamasha la maji maji Selebuka kwa mara ya pili litakaloanza tarehe 28 mwezi Mei hadi tarehe 04 Juni katika viwanja vya maji maji na viwanja vya makumbusho ya Mashujaa wa vita vya maji maji mjini Songea.
Tamasha hili linafanywa kwa lengo la:
1) Kutambua juhudi za shughuli za kiuchumi za wajasiriamali wa mkoa wa Ruvuma kupitia maonyesho ya shughuli za wajasiriamali wadogo wa Ruvuma katika viwanja vya Mashujaa kwa siku saba kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 04 Juni.
Tamasha linalenga pia kupanua soko la wajasiriamali hao kwa watu tofauti kwani kutakuwa na wageni mbali mbali walioalikwa toka ndani na nje ya nchi.
2)Kuibua vipaji na kuviendeleza kupitia michuano ya kimichezo. Kutakuwa na mashindano ya Riadha, na mbio za baiskeli ambazo zitakuwa za aina yake kufanyika mkoani Ruvuma kwa mara nyingine mwaka huu 2016.
Mbio hizi zote zitaanzia uwanja wa majimaji kwenda mpaka peramiho na peramiho kurudi mpaka uwanja wa maji maji tena.
Mbio za miguu zitafanyika siku ya ufunguzi tarehe 28 Mei majira ya asubuhi! Kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha. Kutakuwa na mbio za Kilometa 5, Kilometa 21 na Kilometa 42 na pia tumeongeza mbio za kujifurahisha kwa ajili ya wale ambao wanatamani kushiriki katika riadha lakini wakaosa nafasi katika usahili. Washindi watapata zawadi za pesa taslimu na Medali pamoja na vyeti.
3) Kupeleka mbele elimu kupitia mdahalo ulioandaliwa kati ya shule sita za mkoa wa Ruvuma. Songea Girls, Songea boys, Msamala Sec, Londoni Sec, Kigonsera Sec na Peramiho girls!

MBARONI KWA KUKUTWA AKIFANYA MAPENZI NA MBUZI SONGEA

Picha haihusiani na tukio

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbabroni Rajabu Mbunda(30) mkazi wa kijiji cha Mkumbi wilaya ya Mbinga kwa tuhuma za kukutwa akiwa ndani ya banda la Mbuzi huku akifanya mapenzi na Mbuzi jike.

Akizungumza  Ofisini kwake kamaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi alisema kuwa tukio hilo limetokea januari 18 mwaka huu majira ya saa sita na nusu usiku huko katika kijiji cha Mipeta kilichopo kata ya Mhukulu wilayani songea.

Kamanda Malimi alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Mbunda alikutwa akiwa ndani ya banda la mbuzi  linalomilikiwa na Twaini Mbele(45) mkazi wa kijiji hicho.

Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo hiyo kabla ya tukio mtuhumiwa mbunda aliku amekwenda kwenye nyumba hiyo kwa ajili ya kunywa pombe kwa kuwa kwenye nyumba hiyo kuna klabu cha pombe za kienyeji ambapo alipomaliza kunywa aliaga kuwa anaondoka  na kuacha watu wengine wakiendelea kunywa pombe akiwemo na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye alikuwa anaendelea kuwauzia kinywaji.

Alifafanua zaidi zaidi  kuwa inadaiwa mtuhumiwa Mbunda baada ya kuondoka kwenye kilabu  hicho alielekea kwenye banda la mbuzi ambako baadaye alikutwa na mpita njia huku akifanya mapenzi na mbuzi.

Alieleza zaidi kuwa mpita njia huyo ambaye jina lake limehifadhiwa wakati akipita kwenye eneo hilo la tukio alisikia mbuzi wakipiga kelele na alipowamulika tochi alimuona mbunda akiwa ndani ya banda hilo huku akiwa amemshika mbuzi akiendelea kufanya mapenzi alikimbia hadi kwenye kilabu na kuwaarifu watu waliokuwepo baadaye walilazimika kuongozana naye kwenda na kumkuta mbunda akiendelea kufanya mapenzi na huyo mbuzi.

Alisema kuwa baadaye watu waliokuwa kwenye eneo hilo la tukio akiwepo na mmiliki wa mbuzi huyo walifanikiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho na kumfungia na baadaye walimpeleka kituo cha polisi kwenye kijiji cha Magagula ambao walika na kumchukua na kumpeleka mahabusu.

Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa mtuhumiwa Mbunda ni mkazi wa kijiji cha Mkumbi wilayani Mbinga ambaye inadaiwa alikuwa amekwenda kwenye kijiji hicho oktoba mwaka jana kwa lengo la kutafuta vibarua vya kulima na kwamba muda wowote kuanzia sasa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika.
Na Gideon Mwakanosya –Songeayetu.blogspot.com

BABA AMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WAKE SONGEA


Na Gideon Mwakanosya –Songea Yetu 

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka Mohamed Said Mkazi wa Mjimwema katika halmashauri ya manispaa ya Songea kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike ambaye anasoma darasa la sita katika shule ya msingi Samola iliyopo katika manispaa hiyo.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimezibitishwa na kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma revocatus Malimi zimesema kuwa mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa inadaiwa amekuwa akilawitiwa na kubakwa na baba yake mzazi tangu oktoba mwaka jana .

Malimi alifafanua kuwa inadaiwa saidi alikuwa akimtishia mtoto wake kuwa asiseme kwa mtu yeyote na kwamba taarifa hiyo ikisikika atamuua kwa kuwekewa sumu kwenye chakula au kumchinja kwa kutumia panga.

Alisema kuwa kufuatia vitisho hivyo Saidi anadaiwa kuwa alikuwa akifanya kitendo hicho cha kufanya mapenzi na binti yake mara kwa mara kwani mke wake alikuwa ameachana naye miaka mingi iliyopita.

Alifafanua zaidi kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa mtuhumiwa alikuwa ameachana na mke wake tangu mwaka 2009 na kumuachia mtoto huyo mama yake Hadija Mohamed Hitima mkazi wa Tunduru.

Alieleza zaidi kuwa mpaka oktoba mwaka jana saidi alipolazimika kumfuata mtoto wake alikokuwa anaishi Tunduru na mama yake mzazi kisha kumleta songea ili aendelee kuishi naye.

Kamanda Malimi alieleza zaidi kuwa Saidi alipofika songea mjini alianza kumueleza mtoto wake kuwa anapokwenda kulala usiku asiwe anafunga mlango wa chumba chake na baadaye alianza kuingia kwenye chumba hicho na kuanza kumrubuni na alipoona mtoto anamkataa ndipo alipoanza kumpa vitisho kisha alifanikiwa kutembea naye.

Malimi ambaye pia ni Afisa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Ruvuma alisema kuwa inadaiwa mwanzoni mwa mwezi januari mwaka huu baba mzazi wa mwanafunzi huyo aliaga anaenda shambani ambako binti huyo hakufahamu ndipo mtoto huyo alipata nafasi ya kutoa taarifa kwa majirani ya hali halisi aliyokuwa anafanyiwa ya kufanya mapenzi na kulawitiwa na baba mzazi na baadaye majirani walimsaidia kumpeleka kwenye kituo kikubwa cha polisi cha songea mjini.

Alisema kuwa taratibu za uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zimefanywa licha ya kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa msichana huyo ameingiliwa sehemu zake za siri na mzazi wake  kama alivyojieleza yeye mwenyewe na polisi inaendelea kumsaka mtuhumiwa ili afikishwe mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

MGOMO WA WAFANYABIASHARA SONGEA WADUMU KWA SAA 5

Na Nathan Mtega,Songea

Wafanyabiashara wa maduka wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika kufunga maduka yao kwa zaidi ya masaa matano kwa ajili ya kuzungumza na uongozi wa manispaa na mkuu wa wilayaya Songea kuhusiana na omgezeko la tozo a leseni kwa wafanyabiashara.

Hatua hiyo ya wafanyabiashara kufunga maduka ilifikiwa leo baada yakutokuwepo na makubaliano baina yao na uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Songea ambao ulidaiwa kukiuka makubaliano ya awali ya pamoja yaliyofikiwa baina ya uongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara,uongozi wa manispaa ya Songea na mkuu wa wilaya.

Makubaliano hayo yalikuwa ni kuangaliwa upya kwa viwango vya tozo za leseni vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria ya kodi iliyotungwa na bunge la jamhuri ya muungano ambayo haikuangalia uwezo wa kiuchumi uliopo kwa halmashauri za wilaya,miji na majiji nchini na kwa mzunguko wa fedha uliopo katika mji wa Songea wafanyabiashara waliomba pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo wao kutazamwa kulingsana na mzunguko wa kiuchumi uliopo.

Wakati mazungmzo hayo yakiendelea baina ya viongozi na jumuiya ya wafanyabiashara wa mkoa wa Ruvuma uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Songea uliamua kuendesha msako kwenye maduka kwa ajili ya ukaguzi wa leseni msako ambao ulitumia nguvu zaidi za jeshila polisi kwa kushirikianana askari mgambo kitendo ambacho kiliwafanya wafanyabiashara waamue kufunga maduka yao kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na suala hilo.

Akizungumza katika mkutano huo wa wafanyabiashara mkuu wa wilaya ya Songea Benson Mpesya pamoja na kutumia muda mwingi kuwaomba radhi wafanyabiashara kwa mkanganyiko huo uliojitokeza miongoni mwao na uongozi wa halmashauri wa Manispaa huku akiwaonyeshea kidole wataalamu wa halmashauri ya ya Manispaa kwa kutoa ushauri usio sahihi kwa viongozi wao na kusababisha mkanganyiko huo.

Amesema lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa mfumo ulio sahihi na rafiki kwa kila mmoja na siyo matumizi ya mabavu kwa wafanyabiashara na ili serikali iweze kutoa huduma muhimu kwa wananchi kunapaswa kuwepo kwa mfumo sahihi wa ukusanyaji wa mapato hayo huku akilaani matumizi ya askari wa jeshi la polisi katika ukaguzi huo wa leseni.

 Aidha amewashauri viongozi wa jumuiya ya wafayabiashara na uongozi wa manispaa ya Songea kuimarisha mahusiano chanya miongoni mwao ili kuweza kuijenga manispaa hiyo kiuchumi na pamoja na kushirikiana na mbunge wa jimbo la Songea mjini Leunidas Gama aweze kufikisha kilio hicho cha wafanyabiashara wa manispaa ya Songea cha ongezeko kubwa la tozo la leseni bungeni ili mapitio yaweze kufanyika.

Naye mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiasharawa mkoa wa Ruvuma Titus Mbilinyi aliwahakikishia viongozi wa halmashauri ya manispaa hiyo na mkuu wa wilaya kuwa kuwa wafanyabiashara hawapendi kufunga biashara zao kila wakati na wanatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa bali kinachogomba kwao ni mfumo wa ukusanyaji kodi na kauli za baadhiya watendaji wa mamlaka zilizopo.

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA


Waziri Ummy Mwalimu akisalimiana na Padri Lucius wa hospitali ya Peramiho Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Peramiho, Dr Venance Mushi, alipotembelea hospitali hiyo asubuhi ya leo Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), wakiwa sehemu ya mapokezi, tayari kwa kupata huduma Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiwafariji wagonjwa hospitalini hapo
CDT: JOHN KITIME

Vyandarua vyatumika kuanikia dagaa ziwa Nyasa



Na Gideon Mwakanosya -Mbambay

Baadi ya wananchi wanaoishi katika vijiji vilivyoko kandokando ya ziwa Nyasa katika wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma wamewalalamikia baadhi ya wananchi wakiwemo wavuvi wa samaki kwa tabia yao ya kutumia vibaya vyandarua tofauti na makusudio yake ambapo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  kwa muda mrefu imekuwa ikigawa vyandarua bure lakini baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia kuvulia samaki huku wengine wakitumia kuanikia dagaa kwenye vichanja.


Wakizungumza na NIPASHE, kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Mbaha na Lundu wananchi hao ambao waliomba majina yao yafadhiwe walisema kuwa serikali imekuwa ikigawa vyandarua kwa kila kaya kwa lengo la kupunguza malaria lakini ni jambo la kushangaza baadhi ya wavuvi na wakazi wengine wamekuwa wakitumia vyandaraua hivyo tofauti na ilivyokusudiwa.


Walisema kuwa katika vijiji vingi vilivyoko kandokando ya ziwa Nyasa kumekuwa na tabia hiyo mbaya ambayo inaweza kuhatarisha maisha kwa wakazi wa maeneo hayo ya kuchukua vyandarua kwenye majumba na kupeleka ziwani kuvulia samaki huku wengine wakanikia dagaa wakati wanajua kwamba vyandarua hivyo vimewekwa dawa za viuatilifu.


Wameiomba serikali ya wilaya hiyo kuona umhimu wa kuwazuia au kuwapiga marufuku kuvulia na kuanikia samaki vyandarua na badala yake wananchi wahimizwe kuvitumia vyandarua kama ilivyokusudiwa na serikali na sio vinginevyo. 


Hata hivyo mratibu wa malaria wa mkoa wa Ruvuma, Kibua Amani Kakolwa, alisema kuwa kampeni ya ugawaji vyandarua sehemu za malazi ilifanyika mwaka 2010 ambapo jumla ya vyandarua 706219 viligawiwa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma wakti vyandarua  236375 viligawiwa katika wilaya ya Mbinga kabla kabla wilaya hiyo haijagawanywa.


Kibua alisema kuwa lengo kuu ni kuwa wananchi wanapaswa kuvitumia kila siku ili waweze kujikinga na mbu waenezao malaria na uwezo wa vyandarua hivyo ni miaka mitatu hadi mitano kama vinatunzwa vizuri hivyo watu  wanaoamua kuanikia au kuvulia dagaa wanakwenda tofauti na malengo ya serikali.


Aliongeza kuwa faida ya vyandarua itaonekana katika kupunguza malaria endapo kila mwananchi atatumia chandarua chake kwa usahihi na amezishauri mamlaka za halmashauri za wilaya zitumie sheria ndogo walizo nazo kuhakikisha kuwa wananchi hawatumii vyandarua kwa shughuli ambazo hazikukusudiwa na serikali.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi, aliiambia NIPASHE kuwa ofisi yake ilishapokea malalamiko hayo na kwamba kwa hivi sasa amewaagiza viongozi wote wa serikali wakiwemo maafisa watendaji wa vijiji na kata kuwa mwananchi yeyote atakayepatikana kuainikia dagaa  au kuvulia samaki akamatwe na achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo na maafisa wa idara ya maliasili tayari wameshaanza kufanya msako kijiji hadi kijiji kandokando ya Ziwa Nyasa ili kuwabaini waharibifu wa vyandarua. 


Mwisho      

KADA WA CHADEMA AWASIFIA WABUNGE CCM

Na Gideon Mwakanosya- Songea
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edson Mbogolo, amewamwagia sifa wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndio wawakilishi wazuri na ni wakweli kwa wananchi Bungeni kwani hoja zao wanazozitoa zimekuwa zikileta tija kwa jamii wakiwemo wapiga kura wao.

Hayo yalisemwa juzi (Jumapili) kwenye viwanja vya shule ya msingi Matalawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CHADEMA ambao ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Manispaa hiyo akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe.

Mbogolo aliwataja wabunge ambao alidai kuwa ndio watetezi wazuri wa wapiga kura wao kuwa ni Deo Filikunjombe mbunge wa jimbo la Ludewa mkoa wa Njombe, Kangi Lugola Mbunge wa jimbo la Mwibala mkoa wa Mara na Ally Kessy Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Mkoani Rukwa.

Alisema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiwashangaa wabunge wengi wa CCM ambao wamekuwa wakitoka kwenye majimbo yao kwenda Bungeni bila kubeba hoja za wapiga kura wao badala yake wamekuwa wakitumia muda mwingi kukejeli na kubeza hoja zinazotolewa na wabunge wa upinzani ndani ya Bunge jambo ambalo wanaona ni kitu cha kawaida.
Amewaomba wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali itikadi za vyama vyao vya kisiasa ni vyema wawe wanaona ni muhimu kuwa na hoja zitakazoleta manufaa kwa wapiga kura wao na taifa kwa ujumla na si vinginevyo.

Alieleza kuwa inashangaza sana kuona serikali inaacha kuwabana wabunge wanawaobeza wabunge wenzao wanapotoa hoja zenye tija kwa taifa na badala yake serikali hiyo imekuwa ikitengeneza mazingira ya kuwabana wabunge wa vyama vya upinzani na baadhi ya wabunge wa CCM pale wanapotoa hoja Bungeni walizotumwa kutoka kwenye majimbo yao lakini inaanza mikakati ya kuwabana ili wasiendelee kusema ukweli kwa manufaa ya Taifa.

“Ndugu wananchi ninashangazwa kuona kwamba serikali kupitia ofisi ya Bunge ilifikia uamuzi wa kutaka kuwa mijadala inayotolewa Bungeni isirushwe kwenye luninga jambo ambalo linaonesha wazi kuwa serikali haina nia nzuri ya kuhakikisha kuwa wananchi wanaona kinachofanyika Bungeni”. Alisema Mbogolo.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime akimkaribisha Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ili aweze kuongea na wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara alisema kuwa CHADEMA mkoa wa Ruvuma kwa sasa hivi imejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa mwaka 2015 majimbo yote ya Mkoa wa Ruvuma yatashikwa na wabunge kutoka CHADEMA na alidai kuwa jitihada zinafanywa zaidi kuhakikisha kuwa jimbo la Songea Mjini, linaloshikiliwa na DK. Emmanuel Nchimbi kwa sasa, ni lazima ushindi wa kishindo upatikane.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,  Freeman Mbowe, akiongea na wananchi wa Songea alisema kuwa Watanzania wana haki za msingi kuchagua chama cha siasa wanachokipenda ambacho wao wanaona kuwa ndicho kitakachoweza kuwakomboa na si vinginevyo.

Alisema kuwa Tanzania ina makundi mawili ya uongozi ambapo alilitaja kundi la kwanza kuwa ni la viongozi wanaochaguliwa na wananchi wenyewe ambalo linapaswa kuwa na mamlaka na kundi la pili akalitaja kuwa ni la viongozi wanaoteuliwa na Rais ambalo ndilo linaloonekana kusikilizwa zaidi na kuwa na maamuzi makubwa kutoka serikalini hivyo amewataka wananchi waone umuhimu  kwa sasa hivi kuwa viongozi wote wanaoteuliwa na Rais kama vile wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wanachaguliwa na wananchi na jambo hili liingizwe kwenye katiba mpya.

Alifafanua zaidi kuwa wnanchi katika kila wilaya au mkoa wananchi ni vyema wachague wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kutoka katika  maeneo yao kupitia kwenye vyama vyao vya siasa badala ya ilivyo sasa hivi ambapo wanateuliwa na Rais kutoka katika maeneo tofauti na wanayoongoza.

Aliwataka Watanzania kutambua kuwa mfumo wa siasa wa vyama vingi sio wa ugonvi wala sio wa kuwekeana chuki badala yake vyama vya upinzani ndivyo vinavyoweka bayana changamoto zilizopo kwa serikali inayoongozwa na chama tawala ambayo inapaswa kuzifanyika kazi changamoto hizo.


WATOTO WATANO WALIOZALIWA KWA PAMOJA SONGEA WAFARIKI

Na Julius Konala,Songea
      
WATOTO  wote watano waliozaliwa juzi katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wamefariki usiku wa kuamkia jana .
Watoto hao wote watano walizaliwa salama na Sophia Mgaya (28) mkazi wa Ruhuwiko mjini hapa  kwa kufanyiwa upasuaji  katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma.
Mganga mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Songea(HOMSO)Dkt. Benedict Ngaiza, alisema kuwa watoto hao wameishi kwa masaa kumi tu na kufariki dunia kutokana na  kuzaliwa na uzito mdogo wa chini ya kilo moja.
Dkt.Ngaiza  alibainisha kuwa watoto wote wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo wanakuwa na maisha mafupi,hata hivyo alisema hali ya mama wa watoto hao inaendelea vizuri ingawa bado amelezwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiendelea kupata matibabu.
Tukio ambalo halijawahi kutokea katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma  limetokea Mei 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi  huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa gramu 730,wa pili 810,watatu 670,wanne 820 na watano gramu 430.
Kulingana na mganga huyo kati ya watoto hao waliozaliwa,watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike  na kwamba huu ulikuwa ni mzao wa pili kwa mwanamke huyo.
Alieleza kuwa katika mzao wa kwanza wa mama huyo alifanikiwa kujifungua mtoto mmoja na huu wa pili  amebahatika kujifungua watoto hao watano ambao wote wamefariki dunia .

Mkutano wa CHADEMA waruhusiwa Songea.



Habari tulizozipata hivi punde zinasema Baada ya Mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, hatimaye Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kimeruhusiwa kufanya Mkutano wake wa kampeni ya M4C uliopangwa kufanyika tarehe 26 Mei 2013. Mkutano huo utafanyika Mjini Songea katika eneo la Matarawe Mjini Songea.

Hata hivyo katika makubaliano hayo, CHADEMA imekataliwa kufanya maandamano kama ilivyopangwa awali ambapo ilitangazwa kuwa Mkutano wa hadhara ungetanguliwa na maandamano ambayo yangeanzia katika Chuo Kikuu Huria hadi Matarawe.

Kufutwa na baadaye kuruhusiwa kwa Mkutano wa CHADEMA kumeleta mkanganyiko kwa wananchi wa Manispaa ya Songea kutokana na kubadilika kwa maamuzi ya Dola katika kipindi kifupi.

Habari pia zinaeleza kuwa Baada ya Mkutano wa CHADEMA hapo Mei 26, Chama Cha Mapinduzi CCM pia kitafanya mkutano wake hapa Songea Juni 02, 2013 ambapo Katibu Mkuu wa CCM Abdulahaman Kinana anatarajiwa kufanya Mkutano huo ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi waandamizi wa Chama hicho nchi nzima. Mikutano hiyo ina lengo la kukagua uhai wa Chama pamoja na kutembelea na kuzungumza na mabalozi wa nyumba kumi, viongozi wa mashina ambayo ni uti wa mgongo wa Chama, matawi, kata, wilaya na mkoa.
 

Mwanamke ajifungua watoto watano Songea

MWANAMKE mmoja mkazi wa maeneo ya Ruhuwiko katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Sophia amejifungua watoto watano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Songea, Dk. Benedict Ngaiza, alisema mwanamke huyo alijifungua salama na watoto wake wanaendelea vizuri.
Dk. Ngaiza alisema wauguzi wa hospitali hiyo walimpa huduma nzuri mwanamke huyo jambo lililosaidia kujifungua salama watoto hao licha ya kufanyiwa upasuaji.
Aliongeza kuwa Sophia alijifungua watoto hao jana majira ya saa 4 asubuhi katika hospitali hiyo huku mtoto wa kwanza akiwa na uzito wa gramu 730, wa pili 810, wa tatu 670, wa nne 820 na wa tano gramu 430.
Alifafanua kuwa kati ya watoto hao waliozaliwa, watatu ni wa kiume na wawili ni wa kike na kudai kwamba tukio hilo ni la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ambapo uzao huo ni wa pili kwa mama huyo.
Alibanisha kuwa katika mzao wa kwanza wa mama huyo alijifungua mtoto mmoja

Wakazi wa Manispaa ya Songea walalamikia uchafu uliokithiri

Hili ni moja ya Ghuba lililopo pembezoni ya Mjia wa Songea

 
Ghuba hili lipo mtaa wa mahenge ambalo pia limesahulika kuzolewa taka
  Pichani hapo juu ni ghuba lililopo Mtaa wa Sovi barabara iendayo kituo kikuu cha Polisi likiwa limejaa uchafu .
Wafanya biashara wa Mabucha ya Nyama na wauza Viungo wakiendelea na biashara huku pembeni kukiwa na hali ya uchafu uliokithiri wasiwe na wasiwasi.
.......................................................................
Na Nathan Mtega,Songea
 BAADHI ya wakazi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelalamikia kukithiri kwa uchafu katika maeneo yote ya Manispaa hiyo na kusababisha maghuba ya kuhifadhia taka kufurika kwa muda mrefu yakiwemo yanayozunguka maeneo ya soko kuu,Majengo na kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kuwa mazingira ya usafi kwa ujumla katika Manispaa ni mabaya na yanaweza yakaleta madhara makubwa ya kiafya ikiwa hali hiyo haitachukuliwa hatua za haraka na maafisa afya wa Manispaa hiyo kwa sababu baadhi ya maghuba yamefurika na kutoa harufu kali.

 Walisema kuwa ni muda mrefu hali hiyo ya uchafu imeendelea kuwepo na hakuna jitihada zinazofanyika kuiondoa hali hiyo ambayo ni kero kubwa kwa wakazi walio wengi wa Manispaa hiyo licha ya kuwa wamekuwa wakilipa ushuru wa usafi wa mazingira kila mwezi.

 Wakizungumza Sebastiani Komba na Elizabeth Luambano wakazi wa Bombambili walisema kuwa ni vyema halmashauri ya Manispaa hiyo ikachukua hatua za haraka za kuiondoa adha hiyo ambayo imekuwepo kwa muda mrefu huku Adam Haule na Edson Kumbuka wakazi wa Majengo wakisema kuwa maghuba ya kuhifadhia taka yaliyopo yamefurika kupita kiasi na watoto wakicheza kwenye maghuba hayo hali ambayo inaweza ikawasababishia madhara.

 Naye Seleman Said mfanyabiashara wa soko kuu alielezea kusikitishwa kwake na hali ya kukithiri kwa uchafu ndani ya eneo la soko kuu ambamo kuna ghuba la kuhifadhia taka ambalo ni muda mrefu gali la kuzoa taka halijafika kuchukua taka taka zilizofurika kwenye ghuba hilo na Rashid Husein wa kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea alisema kuwa taka taka zilizopo kwenye ghuba ambalo lipo kando kando mwa kituo hicho zimekuwa kero kwa wasafiri na wapiti njia.

 Afisa afya wa Manispaa ya Songea Maxmilian Mahundi alipojohojiwa na mwandishi wa habari kuhusiana na hali hiyo alikataa kusema chochote kwa madai kuwa yeye siyo msemaji hata hivyo jitihada za mwandishi wa habari zilimtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Nachowa Zacharia ambaye alikiri kukithiri kwa uchafu katika halmashauri hiyo.

 Alisema kuwa halmashauri ya Manispaa ya Songea ina magari mawili tu ambayo ni chakavu na yana zaidi ya miaka ishirini tangu yaliponunuliwa huku mahitaji ya magari mapya kwa ajili ya kuzoa taka ni sita ambayo yana uwezo wa kubeba taka tani ishirini kila moja na kijiko kimoja cha kuzolea taka badala ya kutumia vibarua ambao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kutumia vitendea kazi duni.

 Aidha amewahimiza wakazi wa Manispaa kuendelea kulipa ushuru wa usafi kwa kila kaya ambayo ni shilingi 150 kwa kila siku ili kupunguza adha iliyopo ya uchafu uliokithiri kwenye maeneo mengi ya Manispaa hiyo
Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top