Mh. Joshua Nassari (MB) Chadema |
MGOMBEA
Ubenge Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewashinda wagombea wenzake saba
kutoka vyama vya CCM, AFP, DP, NRA, SAU, UPDP na TLP katika uchaguzi
mdogo wa Ubunge uliofanyika Aprili 1, 2012.
Kwa Mujibu wa Matokeo ya liyotangazwa asubuhi hii yanaonesha kuwa Mgombea Ubunge wa 32,972 26,757.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi.
Gagenzi pia ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walitoka vyama vya Siasa nchini kuwa kama yafuatavyo:-
AFP – 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.
Kwa
mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na
aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa
60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
Aidha CHADEMA pia jana katika Uchaguzi wa Udiwani imepata Ushindi katika Kata za Kirumba mkoani Mwanza na Kiwira mkoani Mbeya.
Post a Comment