Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama hicho jijini Dar es Salaam
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM ameongea na waandishi wa habari kuelezea matumaini yao katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika katka jimbo la uchaguzi la Arumeru mashariki, ambapo chama chake kimeweza kupoteza kiti hicho. Akiwa katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam, ameeleza jinsi walivyojipanga na kushindwa nguvu na wapinzani wao Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA). Uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika jana katika jimbo la Arumeru mashariki, ambapo mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari ameibuka mshindi kwa kupata jumla ya kura 32.972, chama cha mapinduzi kimekubali matokeo hayo yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi leo asubuhi
Nape kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza kijana Nasari na kusema "Tunampongeza Joshua Nasari na hakuna hujuma yoyote juu ya uchaguzi uliofanyika, uchaguzi ulikuwa huru na haki", lakini pia akawapongeza wananchi wa jimbo la Arumeru kwani hiyo ndiyo Demokrasia yao kikatiba
Baadhi ya wandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo leo wakimsikiliza Nape Nnauye alipokuwa akiongea nao juu ya uchaguzi huo kwenye ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam..
Post a Comment