MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoa wa Ruvuma imetupilia mbali ombi la wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali za mitaa 11 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Songea mjini ambao waliitaka mahakama itoe tamko la kuwaengua wagombea wa nafasi hizo kupitia Chanma cha Mapinduzi (CCM) ambao kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2009 walipita bila kupingwa.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Ruvuma Elizabeth Missana alisema kuwa mahakama yake imeangalia pande zote kwa makini na na kusiliza imebaini kuwa wagombea 11 wa nafasi za uenyekiti wa serikali za mitaa kupitia CHAMA CHA MAPINDUZI ambao walipita bila kupingwa ilikuwa ni halali kwasababu katika mchakato wa uchanguzi huo walizingatia kanuni na taratibu za uchanguzi wa serikali za mitaa mwaka 2009.
Hakimu missana alisema kuwa katibu msaidizi wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Songea mjini Zongo Robe Zongo wakati wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ukiwa unaendelea alitoa malalamiko ya pingamizi juu ya uteuzi wa wagombea wa nafasi ya uenyeviti wa serikali za mitaa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wagombea 11 wa nafasi hizo katika mitaa 11 walikosa sifa jambo ambalo mahakama imeliona kuwa lilikuwa ni sahihi.
Alifafanua zaidi kuwa pia mahakama ilibaini kuwa kamati ya rufaa wilaya ya Songea baada ya kupitia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa ilionesha wazi kuwa wagombea wa nafasi ya uenyeviti wa serikali za mitaa 11 katika wilaya ya Songea mjini kupitia chama cha Demokrasia mmna Maendeleo fomu zao za kutaka kuomba kugombea nafasi hizo hazikupishiwa kwenye ngazi za mitaa jambo ambalo linaonekana kuwa ni batili.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo iliyojitokeza mahakama baada yan kusikiliza pande zote imetoa tamko kuwa waliolalamikiwa mahakamani ambao ni wagombea wa nafasi ya uenyetiki wa serikali za mitaa ya Songea kupitia Chama Cha Mapinduzi ndio waliochaguliwa kihalali katika uchaguzi uliofanyika Octoba 25 mwaka 2009.
Alisema kuwa mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote ilifikia maamuzi kuwa msimamizi wa uchaguzi ambae ni mkurugenzi wa halmashauri wa manispaa ya Songea Nachoa Zakaria hakuwaondoa kugombea uchaguzi kwa nafasi walizoomba kupitia Chama Cha Demokrasia Maendeleo kwa kuwaonea na badala yake wagombea hao walipaswa kupeleka malalamiko yao kwenye kamati ya rufaa ya wilaya ya Songea ambayo ndio iliyoengua majina yao na kwamba mahakama imeona kuwa kamati ya rufaa ilikuwa imewaondoa kihalali wagombea 11 kupitia CHADEMA kwasababu hawakufuata maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2009.
Alibainisha zaidi kuwa kila mgombea alitakiwa apate udhamini kutoka ngazi ya chini kabisa ya chama chake cha siasa kitu ambacho hakikufanyika kwa wagombea hao wa CHADEMA na badala yake walipata udhamini kutoka ngazi ya kata na wilaya kutoka kwenye chama chao.
Awali katika mahakama hiyo walitajwa wagombea 11wa nafasi ya uenyeviti wa serilkali za mitaa ambao mahakama imetoa tamko kuwa hawana stahili ya kuwa wagombea kwakuwa hawakutimiza masharti kuwa ni: Innocenti Mgao wa mtaa wa Mdundiko uliopo katika kata ya Mletele, Hamidu Nyalika wa mtaa wa Kotazi uliopo kata ya Majengo, Yusuph Lupindu wa mtaa wa Mahenge uliopo kata ya Mjini na Joseph Mkoma wa mtaa wa Luhila kati uliopo katika kata ya Mwengemshindo.
Wengine ni Prospelia Komba wa mtaa wa Mwengemshindo, Lukulesi Nyoni wa mtaa wa Msafiri uliopo kata ya Matalawe, Said Ligeme wa mtaa wa Kiblang’oma kata ya Lizaboni, Job Mapunda wa mtaa wa Misufini kata ya Mjimwema, Juma Mbalika wa mtaa wa Matomondo uliopo kata ya Mfaranyaki, Omary Kocha wa mtaa wa Mfaranyaki na Rashid Kalulu wa mtaa wa Ruvuma chini kata ya Ruvuma.
Aidha katika mahakama hiyo walitajwa mwenyeviti halali za mitaa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ambao ndio walikuwa wagombea waliopita bila kupigwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Oktoba 25 – 2009, ambao walitimiza vigezo kuwa ni; Mussa Kausia ambae ni mwenyekiti wa mtaa wa Ruvuma chini kata ya Ruvuma, Shaffi Kabirika mwenyekiti wa mtaa wa Mdundiko, Raymond Kawonga mwenyekitiwa mtaa wa Kotazi uliopo kata ya majengo, Joseph Kamba mwenyekiti wa mtaa wa Kibrang’oma kata ya Lizaboni, Gabriel Ndewele mwenyekiti wa mtaa wa Mfaranyaki, Agness Mtega mwenyekitui wa mtaa wa Misufini kata ya Mjimwema, Shamte Omary mwenyekiti wa mtaa wa Mwembemshindo, Alanus Xavery mwenyekiti wa luhila kati kata ya Mwembemshindo, Ahmad Ngaponda mwenyekiti wa mtaa wa Msafiri kata ya Matalawe, Haidiel Mchome mwenyekiti wa mtaa wa Mahenge kata ya mjini na Lufina Mbunda mwenyekiti wa mtaa wa Matomondo kata ya Mfaranyaki.
Pia mahakama imetoa nafasi ya siku 30 kwa walalamikaji ambao wameshindwa endapo wataona mahakama haikuwa tendea haki kukata rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.
Post a Comment