JESHI LA POLISI mkoani Ruvuma
linawasaka watu wanaodaiwa kumbaka mwanamke ambaye jina lake limehifadhiwa
mkazi wa mtaa wa mkuzo katika halmashauri ya manispaa ya Songea na kumsababishia
kifo.
Habari zilizopatikana leo mjini
Songea ambazo zimethibitishwa na afisa mtendaji wa mtaa wa mkuzo manispaa ya
Songea bwana Shaweji Salehe zilieza kuwa mtu mmoja wa jinsi ya kike ambaye
anasadikiwa kuwa na umri wa miaka(32) amekutwa akiwa akiwa ameuwawa na watu
wasiojulikana.
Alisema kuwa baada ya taarifa
hiyo kufika kwenye ofisi yake ndipo alipo toa taarifa ya tukio kwenye kituo
kikuu cha polisi cha mjini Songea ambako alikutana na afisa upelelezi wa makosa
ya jinai wa wilaya ya Songea Inspeta Anna Tembo ambaye alianza kuifanyia kazi
muda mfupi tu baada ya kumjulisha juu ya tukio hilo.
Kwa upande wake kamanda wa polisi
wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Msimeki alipohojiwa leo majira ya
mchana ofisini kwake alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa
limetokea novemba 17 mwaka huu majira ya saa za usiku huko katika eneo la mtaa
wa mkuzo Songea mjini.
Msimeki alifafanua zaidi kuwa
inadaiwa siku hiyo baada ya kutokea tukio hilo majira ya saa 12 asubuhi afisa
upelelezi wa makosa ya jinai wa wilaya ya songea alipokea taarifa kutoka kwa
afisa mtendaji wa mtaa wa mkuzo zilizoelezea kuwa kuna mwanamke ameuwawa na
watu wasiofahamika.
Hata hivyo alifafanua kuwa
uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na
mikwaruzo sehemu za shingoni, pia ilikutwa mipira miwili ya kiume (kondomu) ambayo
ilikuwa imekwisha tumika iliyokuwa imeingizwa sehemu za siri za marehemu huyo
na michirizi ya damu ilionekana sehemu zake za siri kitu ambacho kiliashiria
kuwa mwanamke huyo alikuwa amebakwa na kunyongwa shingo baada ya kumfanyia
kitendo cha kinyama.
Kamanda Msimeki alisema kuwa
uchunguzi zaidi umebaini kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa
miaka miwili iliyopita alikuwa ameolewa na Stambuli Njohopa na baadaye inadaiwa
kuwa walitengana na miezi sita iliyopita mwanamke huyo anadaiwa kuwa alikuwa
anamahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine jambo ambalo linahofiwa kuwa
ndicho chanzo cha mauaji hayo.
Kamanda Msimeki alieleza kuwa
kufuatia kutokea kwa tukio hilo jeshi la polisi mkoani humo wakati linaendelea
kufanya uchunguzi zaidi linawasaka watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo ya
kinyama na kwamba endapo watakamatwa watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka
yanayowakabili.
Post a Comment