BAADHI ya Wagonjwa
waliolazwa katika hospitali ya
Serikali ya Mkoa wa Ruvuma wamelalamikia adha kubwa
ya uhaba wa maji
kwenye maeneo mbalimbali ya
hospitali hiyo ambapo wamedai
kuwa wamekuwa wakilazimika kuyatafuta
maji ya kuoga
au ya kufulia nje
ya hospitali hiyo kwa gharama kubwa.
Wakizungumza na NIPASHE
kwa nyakati tofauti
jana majira ya saa za asubuhi kwenye
Wodi namba 5 na
namba 6 ambazo ni kwa ajili ya
kulaza wagonjwa wanawake baadhi
ya wagonjwa wamesema kuwa kuna
uhaba mkubwa wa maji na
kwamba hakuna hatua zozote ambazo zinaonekana kufanywa
kutatua tatizo hilo ambao limeonekana nia
kelo kubwa.
Wagonjwa hao ambao wameomba
majina yao yahifadhiwe walisema kuwa
tangu walipolazwa hospitalini
hapo wamekuwa wakipata
shida kubwa namna ya kupata
maji hasa wanapohitaji maji
kwa ajili ya
kuoga au kufulia
nguo jambo ambalo
linawalazimu watu wanaowauguza
kutoka nje ya eneo la hospitali hiyo
kwenda kuyatafuta maji yanakouzwa kati
ya shilingi 500 hadi
700 kwa ndoo
moja.
Wagonjwa hao
wameiomba serikali ichukuwe
hatua za haraka
kumaliza tatizo la uhaba
wa maji linalohikumba hospitali
hiyo na kwamb Uongozi
wa hospitali hiyo ni vyema ukaona
umuhimu wa kutafuta
maji hata kwa kuwauzia
wagonjwa waliolazwa hospitalini humo kulio adha
wanayoipata hivi sasa.
Wamsema kuwa tatizo
la kutopatikana kabisa maji
kwenye hospitali hiyo
imekuwa ni kero kubwa
hasa pale wagonjwa wanapohitaji kuoga au
kufua nguo lakini ni
vyema wangewaruhusu wafanya
biashara wanaouza maji kuingia kwenye
mawodi kuuza maji kwa wale
watakao hitaji maji.
Kwa upande wake
Mganga mfawidhi wa hospitali
ya serikali ya Mkoa wa Ruvuma
Dr. Benedict Ngaiza alipohojiwa na
NIPASHE jana mchana ofisini kwake
kuhusiana na hospitali yake kukabiliwa
na uhaba mkubwa
wa maji alikili kuwepo kwa tatizo la
maji ambapo alieleza
kuwa tatizo hilo katika
hospitali yake si kubwa sana
kama wagonjwa wanavyolalamika.
Dr. Ngaiza
alieleza kuwa kumekuwepo
na upungufu wa
maji katika baadhi
ya maeneo ya
hospitali hiyo mfano:
katika kitengo cha maabara
ambako ndiko kuna shida kubwa sana
na kukosekana kwa maji katika kitengo
hicho huduma kwa
wagonjwa hulazimika kusimama
kwa muda wakati
jitihada zikiwa zinafanywa
namna ya kuyapata maji.
Alisema kuwa
kutokana na tatizo
la uhaba wa maji uongozi wa hospitali hiyo
umelazimika kuchimba kisima
cha kuvuta maji
ardhini ambacho kimekuwa kikisaidia
kwa kiasi kikubwa kutoa
maji ambayo yamekuwa yakipelekwa
kwa baadhi ya
maeneo ambayo ni muhimu hospiatalini hapo mfano. Kwenye maabara
na kwenye chumba
cha upasuaji.
Naye mkurugenzi wa maji
safi na maji taka Songea (SOUWASA) muhandisi Frances
Kapongo alipohojiwa na
NIPASHE jana ofisini kwake
kuhusiana na tatizo la uhaba
wa maji alisema kuwa katika
maeneo mengi ya halmashauri ya
Manispaa ya Songea
kumekuwa na uhaba wa maji ikiwa
ni pamoja na eneo la hospitali
ya Mkoa kwa
sababu vyanzo vyote vya
maji vilivyopo katiaka maeneo
ya Luhila na
kwenye milima ya
matogoro vimekauka kabisa na kwamba tatizo hilo litakwisha hadi
muvua zitakapoanza kunyesha na
si vinginevyo.
Post a Comment