Loading...

Mwanafunzi auwawa kwa Radi

Na Gidion  Mwakanosya         Mbinga
 
MWANAFUNZI mmoja Vaileth Tweve (14)  wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Depaul inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Mbinga amekufa papo hapo  na wanafunzi wengine 16 wamejeruhiwa baada ya kupigwa na Radi wakati wakisubiri kupata chakula cha Mchana .
 
Baadhi ya mashuhuda waliiambia KAHAMA FM kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa saba mchana huko katika eneo la Shule ya Sekondari ya Depaul iliopo katika kijiji cha Mbangamawe Wilayani Mbinga  ambako mtoto mmoja wa jinsia ya kike akiwa na wanafunzi wenzake ambao walikuwa wakisubiri kupata chakula cha mchana aliuwawa kwa kupigwa na radi.
 
Mashuhuda hao ambao ni wanafunzi wa Shule hiyo ambao waliomba Majina yao yahifadhiwe walisema kuwa baada ya kuona mwanafunzi mwenzao amepigwa na radi  waliwasiliana na uongozi wa Shule hiyo ambapo jitihada za kuwakimbiza majeruhi kwenda katika hospitali ya wilaya ya Mbinga kwa matibabu zaidi na kwamba maheruhi kumi na sita walilazwa  kwa ajili ya kupata matibabu .
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Oddo Mwisho aliiambia KAHAMA FM jana mjini Mbinga kuwa taarifa ya tukio hilo wameipata juzi majira ya saa tisa alasiri ambapo walikwenda hospitali kuwaona majeruhi kumi na sita na maiti moja iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na alidai kuwa hali za majeruhi zinaendelea vizuri .
 
Naye kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Machael Kamuhanda  amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa lilitokea juzi majira ya saa saba mchana na alimtaja mwanafunzi aliyeuwawa kwa kupigwa kwa radi ni Vaileth Tweve  aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza katika Shule hiyo .
 
Kamanda Kamuhanda alieleza zaidi kuwa inadaiwa tukio hilo lilipokuwa linatokea kulikuwa hamna dalili yoyote ya mvua huku jua likiwa linawaka na wanafunzi wakiwa wanajiaandaa kwenda kupata chakula cha mchana ghafla radi ilipiga na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wanafunzi wengine kujeruhiwa ambao kwasasa wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga .



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top