Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU
wawili wamefariki dunia na wengine watatu akiwemo dereva wa gari hilo
wamejeruhiwa vibaya mkoani Ruvuma baada ya kugongwa na gari katika
eneo la Mahenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea baadaya ya
kugongwa na gari la Jeshi la wananchi (JWTZ) la Makao makuu ya brigedi
Chandamali
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea majira
ya saaa mbili na nusu asubuhi huko kwenye barabara ya Songea na
Namtumbo ambapo aliwataja waliokufa kuwa ni Stumai Moyo (20) na Tabia
Bilali (23) wote wakazi wa eneo la Mahenge wa Songea mjini na walio
jeruhiwa vibaya ni Amina Moyo (2) na Issa Moyo (65) wote wakazi wa
Mahenge ambao baada ya kutokea ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali
ya mkoa ambako wamelazwa
Alifafanua
zaidi kuwa gari hiyo Landlover Discova yenye namba za usajili 1513 JW
97 iliyosababisha ajali na kuuwa watu wawili papohapo na wengine wawili
kujeruhiwa vibaya.
Alieleza
zaidi kuwa gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na MT 97812 SGT Kelvin
Muhagama ilikuwa ikitoka Makao makuu ya Brigedi Chandamali na kuelekea
Songea mjini
Kamanda
Kamuhanda alibainisha zaidi kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi
ambao ilimsababisha dereva wa gari hilo kushindwa kumudu usukani
Naye
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa songea Dr. Mathayo Chanangula
amethibitisha kupokea maiti za watu wawili ambazo kwa sasa zimehifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo na majeruhi
watatu ambao wawili kati yao wamelazwa kwenye wodi za majeruhi na
majeruhi mmoja ambaye ni mtoto wa umri wa mika 2 Amina Moyo amekimbizwa
katika Hospitali ya Mision ya Peramiho kwa matibabu zaidi baada ya
Hospitali hiyo kukosa mashine ya Ex –ray kwani imeonekana kuwa Amina
ameumia kichwani ambako kunahitaji kupata vipimo vya Ex –ray ambapo kwa
sasa hivi huduma hiyo inapatikana katika Hospitali ya Mision ya Peramiho
Dr.
Chanangula alifafanua zaidi kuwa kwa muda mrefu hospitali ya mkoa
songea haina kabisa huduma ya Ex –ray tangu mashine hiyo ilipo haribika
na kwamba kwa hivi sasa wanasubiri mafundi kutoka ufiripino waje
kitengeneza jambo ambalo limeonekana kuwa kero kuwa kwa wakazi wa songea
ambao wamefika kupatiwa huduma hiyo lakini wamekuwa wakielekezwa kwenda
Hospitali ya Mision ya Peramiho ambayo iko umbali wa kilometa 25 toka
Songea mjini
Post a Comment