Loading...

Chama cha soka Ruvuma chapata uongozi mpya

Na Nathan Mtega na Gideon Mwakanosya,Songea NOVEMBA.3.CHAMA cha soka mkoani Ruvuma(FARU) kimefanya mkutano mkuu wa uchaguzi ambapo viongozi wa chama hicho walichaguliwa chini ya katiba ya chama na kanuni za shirikisho la soka nchini(TFF). Katika uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni katibu tawala wa wilaya ya Songea Joseph Kapinga uliendeshwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uchaguzi chini ya mwakilishi kutoka shirikisho la soka nchini Hasan Chabanga ambaye kabla na baada ya uchaguzi alieleza kuridhishwa kwake na jinsi wajumbe na wagombea walivyojitahidi kuheshimu taratibu za uchaguzi. Katika kinyang’anyiro hicho jumla ya wagombea kumi na saba wa nafasi mbali mbali walijitokeza kugombea huku nafasi ya mwenyekiti ikigombewa na wagombea watatu ambao ni Golden Sanga aliyeibuka mshindi kwa kupata kura 17 dhidi ya Joseph Mapunda aliyepata kura 15 huku mgombea wa tatu Damas Ndumbaro akijitoa kabla ya uchaguzi huo. Katika nafasi ya makamu mwenyekiti Zuberi Kivo aliibuka mshindi kwa kura 24 dhidi ya mgombea mwenzake Hussein Ndimbo aliyepata kura 8 na nafasi ya katibu mkuu ikichukuliwa na Ahmad Challe aliyepata kura 17 huku mgombea mwenzake Henry Kabera akipata kura 15 na nafasi ya katibu mkuu msaidizi ikichukuliwa na Ajaba Chitete kwa kura 14 huku mgombea mwenzake Mark Mapunda akipata kura 12. Nafasi ya mweka hazina iligombea na mmoja Deogratias Liganga aliyepigiwa kura za ndiyo 29 huku kura mbili zikimkataa na nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu taifa ikichukuliwa na Humphrey Milanzi kwa kura 24 baada ya kuwabwaga wagombea wengine ambao ni Benjamin Mwakasonda,Rahid Luena na Mohamed Gayo. Aidha nafasi ya ujumbe wa Kamati ya utendaji ya chama hicho cha soka mkoa iligombewa na wagombea wawili ambapo Emmamuel Kamba alipata kura 24 na Kelvin Haule akipata kura 25 na kwa mujibu wa katiba ya chama cha soka mkoa wa Ruvuma bado kuna nafasi moja wazi ya mjumbe wa Kamati ya utendaji wa chama hicho na James Mhagama alifanikiwa kutetea nafasi yake ya mwakilishi wa vilabu kwa kupigiwa kura 29 za ndiyo kati ya kura 32 zilizopigwa. Baada ya msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo hayo katika hali isiyokuwaya kawaida mgombea Joseph Mapunda aliinuka na kwenda kumkumbatia mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti Golden Sanga na kutamka kuwa alikubali matokeo na atakuwa tayari kushirikiana na uongozi uliochaguliwa naye mwenyekiti wa chama cha soka mkoa mbali ya kuwashukuru wapiga kura kwa kumchagua lakini alihahidi kuendeleza ushirikiano kwa lengo la kuendeleza soka mkoani Ruvuma.


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top