Loading...

RC MWAMBUNGU AHIMIZA WANANCHI KUKOPA MATREKTA

Serilikali mkoani Ruvuma imeweka mikakati ya uzalishaji zaidi wa mazao ya chakula ili kuweza kujitosheleza zaidi na kutoa ziada kwani katika msimu wa 2010/2011 mavuno ya mazao mbalimbali ya chakula ambao chakula chake kinatumika msimu wa 2011/2012 yalikuwa tani 1211348 ikiwa wanga tani 1168538 na utamwili tani 42812.
Hayo yalisemwa jana na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wakati akizungumza ofisini kwake ambapo alifafanua zaidi kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2011/2012 mkoa wake umepanga kulima jumla ya hekta 595001 za mazao ya chakula na biashara zilizotarajiwa kuwa na mavuno ya tani 1278551 na mazao ya biashara ni hekta 125422 zitakazotoa mavuno ya tani 54741 kutakuwa na ongezeko la eneo la kilimo la asilimia 6.1 na ongezeko la mavuno asilimia 2.
Mwambungu aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa kazi kubwa ya uzalishaji waliofanya na kwamba wanayoendelea kuyafanya katika mazao yote likiwemo zao la mahindi ambapo wamedhihirisha kwa vitendo kuwa sera ya kilimo kwanza mkoani Ruvuma imefanikiwa.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo yaliyotajwa mkoa wake umeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali kwakuhakikisha mahindi ya ziada ya wakulima yote yananunuliwa na serikali au wafanyabiashara wakubwa. Alibainisha zaidi kuwa katika msimu wa kilimo wa 2010/2011 wakala wa wahifadhi ya chakula ya Taifa (NFRA) mkoani Ruvuma ili waweza kununua tani za mahindi 52100 zenye thamani ya shilingi bilioni 18.2 ambazo ikichanganywa na mahindi yaliyonunuliwa msimu 2009/2010 zilifikia wastani wa tani 92500 zilizohifadhiwa kati ya tani 88000 zimesafirishwa kwenda maeneo yenye uhaba wa chakula kama Dodoma, Dar es Salaam, Iringa na nchini Uganda.
Hata hivyo mkuu wa mkoa Mwambungu alisema kuwa ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula mkoani humo ofisi yake imeshafanya mawasiliano na shirika la uzalishaji la mali la jeshi la kujenga Taifa (SUMA JKT) ambapo mawasiliano hayo yamekwishafanyika na kufikia maafikiano kuwa kuanzia wakati wowote matrekta zaidi ya 50 yataletwa ambayo yatakopeswa kwa wakulima kwa awamu kwa kipindi cha miaka minne yaani deni litalipwa kwa kila baada ya mwaka mmoja kwa miaka mine ambalo ni shilingi milioni 14 hivyo amewahimiza wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya na manispaa kuhakikisha kuwa wana wahimiza wananchi wa kiwemo wakulima kuona umuhimu wa kuyakopa matretka ili waondokane na kilimo cha kutumia jembe la mkono ambalo linazoroteshauzalishaji.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top