Loading...

WANACHUO WA ST. AUGUSTINE SONGEA WAFANYA BONANZA

Wanafunzi wa chuo kikuu ST. Augustine tawi la Songea Jumamosi ya wiki hii walifanya bonanza lenye lengo la kujenga mwili na kuweka akili sawa kabla ya kuanza mitihani ya mwisho wa semesta siku chache zijazo.

Michezo iliyofanywa katika bonanza hilo ilikuwa ni mpira wa pete, kuvuta kamba, kukimbia katika magunia na kukimbiza kuku. Timu zilizoshindana ni timu ya wanafunzi wa lugha na timu ya sayansi jamii.


Mikikimikiki katika pambano la mpira wa pete


Timu ya lugha ikiisurubisha timu ya sayansi ya jamii

Washindi wa mpira wa pete wakikabidhiwa zawadi ya mbuzi
Mkuu wa chuo, wahadhiri na baadhi ya mashabiki wakifuatilia pambano la mpira wa pete
Wengine walijikumbushia enzi za utoto wao kwa kuruka kamba

Wanaume wakijiandaa kukimbia katika magunia

Mbio za magunia zikiendelea

Wanawake wakijiandaa kukimbia katika magunia
Mshindi wa mbio za magunia kwa wanawake
Vidume vikioneshana ubabe katika kuvuta kamba

Wanawake wakijiandaa kuvuta kamba
Mshindi wa kukimbiza kuku akiwa amebebwa juu na mashabiki wakePost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top