Loading...

Watu wanne wakamatwa na kilo 360 za bangi Songea


WATU wanne akiwemo fundi seremala wanashikiliwa na polisi mkoani Ruvuma katika matukio mawili tofauti kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogramu 360 iliyokuwa ikisafirishwa kwa pikipiki kutoka vijiji vya Mpepai wilayani Mbinga na Matomondo wilayani Songea vijijini kwenda Lizaboni katika halmashauri ya manispaa ya Songea kuiuza.

Akizungumza  ofisini kwake kamanda wa polisi wa mkoani Detidelit Msimeki awataja watuhumiwa hao kuwa ni Willy Njogopa (30) mkazi wa Lizaboni manispaa ya Songea, Hamis Chenda (24), Aron Ngongi (30) na Bethod Henjewele (30) ambaye anajishughulisha na kazi ya ufundi seremala na wote ni wakazi wa kijiji cha Litapwasi kilichopo halmashauri ya Songea vijijini.

Kamanda Msimeki alilitaja tukio la kwanza kuwa lilitokea juni,26 mwaka huu majira ya saa 1.00 usiku huko katika kijiji cha Matomondo ambako askari polisi wakiwa dolia walimkamata Njogopa akiwa na bhangi yenye uzito wa kilogramu iliyokuwa imehifadhiwa ndani ya kiroba ambacho kilikuwa kimefungwa kwenye pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili T904 BMV iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa Ngongi.

Alifafanua zaidi kuwa askari polisi ambao walikuwa wakitoka katika kituo kikuu cha polisi cha Songea kwenda katika kijiji cha Magagula wakiwa njiani ghafla walimwona Njogopa akiwa anaendesha pikipiki ambayo ilikuwa imebebea furushi kubwa na waliposimama Njogopa alianza kutaka kukimbia lakini baadae walifanikiwa kumkamata, na walipomhoji alikiri kuwa pikipiki ni mali yake lakini mzigo uliokuwa umefungwa nyuma ya pikipiki hiyo aliukana kuwa si mali yake lakini walimkamata na kuondoka nae kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kufanya nae uchunguzi zaidi.

Kamanda Msimeki alilitaja tukio jingine kuwa lilitokea juni 27 mwaka huu majira ya 1.00 usiku huko katika kijiji cha Mpepei wilayani Mbinga askari polisi wa kituo kikuu cha polisi wilayani Mbinga wakiwa dolia walifanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na bhangi yenye uzito wa kilogramu 300.

Alieleza zaidi kuwa bhangi hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika maroba matatu na vifurushi vidogo vitatu vilivyokuwa vimefungwa kwenye maroba matatu yaliyokuwa yamebebwa kwenye pikipiki tatu tofauti ambazo namba zake za usajili ni T696 BSJ aina ya SANLG, T729 BPT aina ya SANLG na T195 ARC aina ya SANLG.

Hata hivyo kamanda Msimeki alisema kuwa watuhumiwa wote wamekamatwa wakiwa na vielelezo na ni watumiaji na wauzaji maarufu wa madawa hayo ya kulevya aina ya bhangi na kwamba jeshi lake la pilisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na matukio yote mawili yanayowakabili.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top