WATU wawili mtu na mkewe katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua kinyama kwa kumpiga kwa mawe mtoto wao mchanga wa Miezi saba na kumuweka kwenye Chemba ya Mtaro wa maji kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Masuala ya kimapenzi.
Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Chemchem katika Kata ya Matogoro Mkoani humo, Fama Suta amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Shangwe Komba(28) na Mkewe Mwazani Chimgege(25) wakazi wa Chemchem Matogoro Mkoani humo.
Amewaambia Waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Julai 16 mwaka huu katika Mtaa wake ambapo anasema yeye baada ya kufahamishwa kuhusiana na tukio hilo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Mjini kati kwa njia ya simu.
Kiongozi huyo wa Mtaa akisimulia jinsi tukio lilivyosikitisha alisema kuwa kwa jinsi tukio lenyewe alivyoliona, awali mtoto huyo wa kiume inasemekana alinyweshwa sumu na kunyongwa na kisha kupigwa mawe akiwa kwenye Mtaro wa Chemba ya kupitishia maji. .
Alieleza zaidi kuwa mtoto huyo wiki mbili zilizopita alifanyiwa tohara na kwa kweli ni tukio linalosikitisha ambapo mimi linanifanya niweweseke usiku na katika Mtaa wangu hili ni tukio la kwanza’alisema na kuongeza
Polisi walimkamata Zawadi Komba dada wa Mtuhumiwa Shangwe Komba na kumuhoji kuhusiana na tukio hilo ambapo alieleza kuwa mdogo wake huyo alimuomba ampe sh. 50,000 akamtibu mwanae huyo wa kufikia aliyemuua.
Hata hivyo baada ya kumuhoji Mwanamke huyo na kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa kwa ushirikiano wake Polisi walimuachia huru.
‘Kwa kweli inaonyesha kuwa Mwanaume huyo alishauriana na Mkewe wamuue mtoto huyo ili waweze kufurahia maisha yao katika mapenzi na kutafuta mtoto mwingine kwa kuwa mtoto yule hakuwa wa Mwanaume huyo’alisema.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma,Deusdeliti Msimeki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini chanzo chake na kuwafikisha Mahakamani Wathumiwa.
Post a Comment