WAKATI sakata la madaktari likiwa linaendelea hapa nchini Mkoa wa Ruvuma unakabiliwa na tatizo kubwa la uhaba wa madaktari ambapo Mpaka sasa kuna madaktari 87 wakiwemo madaktari bigwa 11 wakati idadi hiyo ya madaktari waliyopo ni ndogo haitoshi kumudu shughuli za kutoa huduma za afya kwa ufanisi zaidi kwa wagonjwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake mganga mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela alisema kuwa Mkoa wa Ruvuma bado unaidadi ndogo ya madaktari ambao pamoja na kuwepo na mazingira magumu wamekuwa wakiendelea kufanya kazi zao bila kuwepo na usumbufu wa anina yeyote. Dr. Malekela alisema kuwa Mkoa wa Ruvuma tangu kuwepo kwa manung’uniko ya Madaktari lakini wagonjwa wamekuwa wakiudumiwa tofauti na maeneo ya mikoa mingine imekuwa ikisikika kuwepo na migomo na badala yake umekuwepo na ushauri wa mara kwa mara wakuwataka madaktari kuwa wavumilivu pale wanapoendela kudai baadhi ya mambo ambayo yangeweza kuboresha zaidi huduma ya afya. Alifafanua zaidi kuwa Mkoa wa Ruvuma unahospitali 10 kati ya hizo hospitali 4 ni za serikali ambazo alizitaja kuwa ni Hospitali ya serikali ya wilaya ya Mbinga,Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Namtumbo na hospitali ya serikali ya Mkoa. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Malekela alizitaja hospitali binafsi zilizopo Mkoani humo kuwa ni Hospitali ya Misheni ya Peramiho,Hospitali ya Misheni litembo,Hospitali ya Misheni ya Mbeza,Hospitali ya Misheni Lituhi,Hospitali ya Misheni ya Liuli, Hospitali ya Misheni ya Kiuma na Hospitali ya Misheni ya Luanda. Alisema kuwa kutokana na hali hiyo changamoto kubwa iliyopo kwenye hospitali hizo ni idadi ya madaktari ni ndogo na haikidhi kumudu Shughuli za kutoa huduma za afya za ufanisi kwa wagonjwahivyo ameiomba serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kuona umuhimu wa kuongeza idadi ya madaktari Mkoani Ruvuma kwa lengo la kuborehsa zaidi huduma hiyo kwa wagonjwa. |
Loading...
Home » Unlabelled » WAKATI SAKATA LA MADAKTARI LIKIWA LINAENDELEA MKOA WA RUVUMA WADAIWA KUKABILIWA NA UHABA MKUBWA WA MADAKTARI
Post a Comment