Loading...

WAKATI MKOA WA RUVUMA UNAKABILIWA NA VIFAA VYA SENSA MAKALANI NA WASIMAMIZI WAGANGA NJAA

Na Gideon Mwakanosya, Songea


WAKATI zimebaki siku chache za zoezi la makazi ya watu Mkoa wa Ruvuma bado unakabiliwa baadhi ya changamoto zikiwemo za uhaba wa vitabu vya mageresho,madodosho na kuto kuwalipa baadhi ya malipo makalani na wasimamizi wa zoezi la sensaWakizungumza na kwa nyakati tofauti jana mjini Songea baadhi ya makalani na wasimamizi wa sensa katika Halmashauri ya manispaa Songea ambao waomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa pamoja na kwamba siku zimebaki chache za kuanza zoezi la sensa lakini bado kunachangamoto zinazoonyesha kuwepo kwa ugumu wa zoezi hiloWalisema kuwa katika eneo hilo la manispaa ya songea kuna uhaba mkubwa wa vitabu, magersho na madodoso na kwamba hata wakati wa mafunzo bado kulikuwa na uhaba wa vifaaWalifafanua zaidi kuwa hata malipo kwa makalani na wasimamizi wa sensa walilipwa kwa awamu mbili tu lakini malipo kwa ajili ya kwenda kutambua maeneo ya kuhesabia mpaka sasa fedha hzo hazijatolewa kwa makalani na wasimamizi na kwamba uandikishaji wa daftari la makadhi mpaka sasa bado posho yake haifahamiki.Walieleza zaidi kuwa wamejalibu kutoa malalamiko juu ya posho zao lakini mpaka sasa hakuna maelezo yenye majibu kamili licha ya kuwa wamekuwa wakihimizwa kwenda kwenye maeneo yao ya kazi huku wakipewa ahadi fedha zao watakuja kulipwa baadaye.Kwa upande wake mratibu wa sensa wa mkoa wa Ruvuma John Lyakurwa alipohojiwa jana ofisini kwake alikili kuwa badhi ya vifaa vilishaletwa na kwamba vifaa vingine vinatarajiwa kuletwa kwa ndege ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Alifafanua zaidi kuwa vifaa vya zoezi la sensa vinavyotarajiwa kuletwa ni pamoja na mabegi maalum yatakayo tumika kuhifadhia madodoso na baadhi ya nyaraka ambazo zilikuwa bado hazijaletwa ambazo zimekosekana kwenye madodoso yaliyopo.Alibainisha zaidi kuwa vitabu vya malegesho ndio tatizo kubwa ambalo lipo ambapo imelazimika kuazima vitabu hivyo kwa mratibu wa sensa wa mkoa wa Iringa ambavyo vinatajiwa kuletwa wakati wowote kuanzia sasa ili kukidhi tatizo hilo .Alisema mahitaji ya vitabu ya malejesho mkoani Ruvuma ni 4117 lakini vitabu vilivyo letwa ni 600 wakati makalani wa sensa kwa mkoa wa ruvuma wako 4300 na wasimamizi wako 320 na kwamba fedha za posho wanazo dai serikali itawalipa na wajaribu kuiwa na subira na posho ya uwandikishaji wa daftari ya makazi imeandaliwa kwa muda wa siku tatu kwani serikali italipa 50000 kwa kila sikuNaye mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu alipohojiwa jana ofisini kwake kuhusiana na matatatizo hayo alisema kuwa serikali inajitahidi kwa kila hali kuwa zoezi la sensa linafanyika na kwamba makalani wa wasimamizi serikali itawalipa malipo yao.
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top