Loading...

MWANAMKE ACHOMWA PASI MWILI MZIMA BAADA YA KUTEMBEA NA BABA MKWE WAKE MARA TATU

chanzo freebongo.blogspot.com
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Henry amejikuta mikononi mwa vyombo vya dola baada ya kumchoma mkewe sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia pasi na kumuua mtoto wake wa mwaka mmoja kwa madai kuwa mwanamk huyo amekuwa akitoka kmaenzi na baba yake mzazi........ Akiongea kwa majuto makali huku akiwa "nyuma ya nondo", Henry anadai kuwa alifanya hivyo bila kukusudia "Nakiri kwamba nilifanya maamuzi ambayo sikutegemea kuyafanya katika maisha yangu.Nilikuwa napandwa na hasira kubwa kila nikimuona yule mtoto akiamka na kulilia maziwa . Moyo ulikuwa ukijaa nakunifanya nishindwe hata kupumua na ndipo siku moja ndani ya moyo wangu nilisikia sauti ikiniamuru nimuue yule mtoto maana si damu yangu. Bila kujizuia, nilimshika shingoni, nikamkaba na kumpiga kwa nguvu......." Henry alielezea tukio hilo huku aimwaga machozi ya uchungu "Najua kuanzia sasa maisha yangu yatakuwa ni gerezani tu.Nakubaliana na yote ila nimeona ni bora jamii iujue ukweli....... Mke wangu Mercy alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na baba yangu mzazi .Kabla ya tukio hili, nimekuwa nikimuonya mara nyingi sana kwamba aache tabia hiyo na asiende nyumbani kwa baba maana nilikuwa nimeshausoma mchezo huo.Mbaya zaidi mke wangu hakutaka kunisikiliza..... Siku moja mke wangu aliaga kuwa anataka kwenda kwa rafiki yake.Nilimkataza na kumwambia kuwa asitoke wala kwenda kokote lakini hakunisikia.Baada ya muda kidogo nilizuga na kumwambia kuwa natoka kidogo.Baada ya nusu saa nilirudi nyumbani na sikumkuta mke wangu..... ....Nilisubiri kidogo huku akili ikiwa haifanyi kazi.Baadaye moyo ulinituma kuwa niende kwa baba nikamuangalie maana si mbali sana kutoka nyumbani........ Nilifika na kugonga mlango.Baba alitoka akiwa amejifunga taulo tu.Nilipojaribu kuingia ndani alinizuia.Baada ya kuzozana naye kwa muda niliamua kuacha na kurudi nyumbani.......Sijui mke wangu alitorokaje na kuniwahi kufika nyumbani, lakini niliporudi nilimkuta ameshafika. Badala ya kuchukia, nilijiuta nacheka sana .yaani nilikuwa kama mtu aliyerukwa na akili.Nilijisogeza pembeni na kuanza kuvuta sigara ili kupunguza hasira...... Ilipofika usiku, nilichukua nguo yamteja wangu na kuanza kuipiga pasihuku nikiwa na mawazo mengi.Baadae nilisikia sauti ndani ya moyo wangu ikiniambia nijikaze japo nimulize ili niujue ukweli.Wakati huo pasi ilikuwa ni ya moto kwelikweli. Ghafla maamuzi yakaniijia kuwa niitumie ile pasi kumtisha ili aniambie ukweli wa tukio zima...... Nilimsogelea na kumwamsha.Alipoamka nilimuomba anieleze ukweli tena kwa nia nzuri kabisa.Mercy hakunijibu kitu na badala yake alikaa kimya.Nilijawa na hasira na kujikuta namchoma kwa kutumia ile pasi Nilipofanya vile,Mercy alikiri kuwa amewahi tembea na baba yangu mara tatu.....Aliposema vile hasira zilinipanda zaidi na kujikuta namchoma zaidi...... Wakati nafanya vile,mtoto aliamka na kuanza kulia kama ishara ya kutaka kunyonya.Nilimwangalia kwa hasira huku moyo ukiniambia kuwa yule si mwanangu...." Henry alikaa kimya kwa muda huku akiwa amejiinamia.Baada ya muda kidogo alinyanyua kichwa na kuangalia juu huku uso wake ukiwa umelowa machozi.... Baada ya kimya cha muda, Henry aliendelea kwa kusema kuwa:"Yalikuwa ni maamuzi mabaya sana.Wakati yule mtoto akilia, nilimshika na kumkaba shingo.Baada ya kumkaba nilimpiga kwa ngumi. Wakati najiandaa kumpiga mara ya pili, mke wangu aliudaka mkono wangu.Nilipoona ameshika mkono, nilitumia mkono mwingine kumuunguza zaidi huku mkono mwingine ukiendelea kumpiga mwanangu.....Mwanangu hakuweza kutoa sauti tena."Alimalizia Henry huku akilia kwa sauti kubwa


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top