Na Gideon Mwakanosya, Songea
BAADHI ya madereva na wamiliki wa vyombo vya moto wakiwemo waendesha pikipiki (bodaboda) katika halmashauri ya manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamepongeza juhudi za mkuu wa wilaya ya songea Joseph Mkilikiti za kusimamia kwa makini uuzaji wa mafuta katika vituo vya Mdaula na Kisumapai na kuwabana baadhi ya watu wabaya wanaotaka kununua mafuta hayo kwa wingi wakati wanajuaq kunauhaba mkubwa wa mafuta na kwenda nayo vijijini kwenda kuyayuza kwa bei kubwa sana.
Pongezi hizo zimetolewa jana wakati mkuu huyo wa wilaya hiyo Mkilikiti alipokuwa kwenye maeneo ya vituo hivyo ambavyo vipo kandokando ya kituo kikuu cha mabasi ambako alifika kusimamia kuwa kila mtu aliyefika kununua mafuta akiwa na gari anapewa lita 5 za dizeli na petrol na mwenye pikipiki unapewa lita 2 za mafuta hayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti madereva na wamiliki wa vyombo vya moto walisema kuwa kufuatia kuwepo kwa uhaba mkubwa wa mafuta kwenye vituo vyote vya kuuzia mafuta mkoani Ruvuma ambako kumesababisha mafuta aina ya dizeli na petrol kuadimika kabisa na kuwepo mianya baadhi ya walanguzi kuyauza kwa bei kubwa kati ya shilingi 5000 mpaka 6000 kazi aliyoifanya mkuu wa wilaya ya kuzuia watu wasinunue mafuta kwa uwingi inastahili pongezi kubwa
John Haule mkazi wa Mfaranyaki ambaye ni mmoja wa waendesha pikipiki aliimwambia mwandishi wetu kuwa, kwa sasa hivi katika vijiji vya Muhukulu .Mpitimbi, Mgazini na maeneo mengi ya vijiji mafuta hayo yamekuwa yakiuzwa kwa bei mbaya hivyo kitendo alichokifanya DC Mkilikiti ni cha busara sana kwani kunabaadhi ya walanguzi walikuwa wakinunua mafuta kwa wingi na kuyapeleka vijijini kuyauza kwa lita mmoja kati ya shilingi 5000 na 6000 .
Mmoja wa wamiliki magari ambaye hakutaka jina lake litajwe alieleza kuwa upatikanaji wa mafuta ni mgumu sana lakini anashangaa kuona kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakinunua mafuta kwa wingi na kwenda kuyauuza nje ya manispaa kwa bai kubwa.
Mwandishi wetu ameshuhudia mkuu huyo wa wilaya Mkilikiti akiwa kwenye kituo cha kuuzia mafuta cha mdaula ambako kulikuwa na msongamano mkubwa wa pikipiki na magari akiwasimamia wauzaji mafuta kuhakikisha kila mwenye pikipiki anauziwa lita 2 za mafuta na wenye magari ni lita 5 za mafuta .
Akizungumza kwenye eneo hilo la mafuta Mkilikiti alisema kuwa kunauhaba wa mafuta katika vituo vyote vya mafuta lakini kwa vile kunakiasi kidogo cha mafuta yamekuja kwenye vituo viwili ni lazima mafuta hayo yauzwe kwa wafanya biashara wa waendesha pikipiki na wenye magari lakini amewaonya baadhi ya watu wenye tabia mbaya wanaochukulia nafasi tatizo hilo na kwenda kuyauza mafuta kwa bai kubwa ambayo ni zaidi ya mara mbili ya bei ya mafuta na yeyote atakayekamatwa ataona ubaya zaidi ya mkono wa dola.
Alisema kuwa amewaagiza maafisa watendaji wa vijiji na wa kata kuhakikisha kuwa wanawadhibiti watu wabaya wanaouza mafuta huko vijijini kwa bei kubwa na kwamba wakiwaona wawakamate na wawapeleke ofisini kwake wakaonje joto la jiwe .
Kwa upande wake meneja wa kampuni ya usafirishau na uuzaji wa mafuta ya mdaula tawi la Songea Faustin Kamhabwa alisema kuwa mafuta yaliyopo ni kidogo sana ambapo alifafanua kuwa mafuta aina ya disel zimebaiki mita 700 na petrol zimebaki mita 500 na mafuta ya taa hakuna kabisa .
Naye mmoja wa wawafanyakazi wa kituo cha mafuta cha kisumapai Focus Inju alieleza kuwa tatizo la mafuta ni kubwa na kwamba mafuta yaliyopo hayatoshelezi mahitaji ya wakazi wa songea na kwamba kwa sasa kunatatizo kubwa zaidi la mafuta ya taa jambo ambalo limeonekana kwa ni kero kubwa sana.
Loading...
Post a Comment