Loading...

MWENYEKITI WA KIJIJI KYELA AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA NA RADI

Mwenyekiti wa kijiji cha Mbako tiketi ya ccm amefariki dunia baada ya kupigwa na radi,akizungumza na mwandishi hizi mke wa marehemu bi Mbutolwe kakonyole amesema kuwa yeye alikuwa nje ya nyumba yao huku mumewe marehemu Wyine Mwakaleja akiwa ndani na watoto wao wawili akiwa anapata chakula. Amesema kuwa baadaya muda kidogo kupita tangu yeye akiwa hapo nje radi kubwa ikapiga na kupelekea yeye kuanguka chini na kupoteza fahamu ,na alipo zinduka akabaini kuwa mumewe hajaja pale kumpa msaada wowote pamoja na kupiga kele za kuomba msaada . Ameendelea kusema kuwa akaamua kujikongoja hadi ndani ambako alimkuta mumewe akiwa amelala chini huku anatetemeka ndipo akatoka nje na kuanza kupiga mayowe ya kuomba msaada toka kwa majirani na majirani walipofika wakaamua kumchukua marehemu Wyine na kutaka kumuwahisha hospitali ya wilaya ya Kyela lakini jitihada zao ziligonga mwamba kwani marehemu alikata roho kabla ya kufikishwa hospitali. Baba mzazi wa marehemu bwana Ibrahim Mwaikana amesema kuwa ameshitushwa sana na taarifa za kifo cha mtoto wake huyo kwani muda si mrefu sana tangu kifo hakija mpata alikuwa naye pamoja wakipanga mambo frani juu ya familia dakika chache tu baada ya mipango yao hiyo akawa anapokea taarifa za kifo cha kijana wake Wyine kitu kilichomfanya ashindwe kuamini. Afsa mtentaji wa kijiji hicho amekili kutokea kwa kifo hicho na amesema mazishi ya bwana Wyine wakaleja yalifanyika tarehe 2/11/2012 saa nana mchana na ameongeza kuwa kifo cha bwana huyo ni pengo kwa kijiji kizima cha Mbako kwani alikuwa ni mwenyekiti mchapa kazi na mpenda maendeleo si majungu.


Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top