Loading...

UCHAFU WAENDELEA KUUTESA MJI WA TUNDURU

ABIRIA wanaosafiri kutoka na kuingia katika Kituo cha kikuu cha Mabasi
Mji wa Tunduru Mkoani Ruvuma wamelelemikia kukidhiri kwa Uchafu
katika kituo hicho.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na Waandishi wa Habari kwa mashariti ya
kutotajwa majina yao, wananchi hao walisema kuwa mbali na kuwepo kwa
utaratibu wa halmashauri ya Wilaya hiyo kuwatoza ushuru kwa magari
yanayo egeshwa katika kituo hicho lakini kumekuwa hakuna juhudi zozote
za kufanyika kwa usafi

Katika taarifa hiyo wananchi hao walisema ushuru ambao hutozwa ni Tsh.
1000 kwa kila gari linalo ingia na kutoka katika kiyuo hicho, na
magari  yanayo egeshwa ndani ya kituo hicho yakitozwa Ths.1000 kwa
kila gari linalo egeshwa haubuhi.

Aidha abiria hao pia walielezea kubainisha baadhi ya adha wanazo
zipata kutokana na uchafu huo walidai kuwa mbali na kuenea kwa uchafu
huo katika eneo la kituo hicho pia wamekuwa wakikerwa na harufu
katika miwambaza vya kituo hicho hali inayo onesha kuwa watumishi wa
idara ya afya wameutelikeza mji huo kikiwemo kituo hicho cha mabasi.

Abiria hao waliendelea kueleza kuwa kitu kingine kinacho wakwaza
abiria hao ni pamoja na kushamiri kwa uchafu katika vyoo ambavyo
hutumiwa na abiria hao na maeneo mbali mbali ya Biashara katika
mighahawa na mabaa yameonekana kukidhiri kwa uchafu.

Jitihada za kumpata afisa afya wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
aliyefahamika kwa jina moja la  Muhagama ziligonga mwamba baada ya
simu yake kupigwa zaidi ya mala 5 ili aweze kuzungumzia juu ya
kukithiri kwa uchafu katika kituo hicho na mji huo kwa ujumla.

Hata hivyo alipoulizwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo Robert Nehatta mbali na kukiri kukidhiri kwa uchafu huo alisema
kuwa chanzo cha uchafu huo kimetokana na kukosekana kwa mafuta ambayo
yangetumika katika magari ya kubebea takataka hizo.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari umebaini kuwa mafuta ni
tatizo la kudumu katika wilaya hiyo na kwani hadi sasa halmashauri hiyo
haina magari ya kubebea taka na kwa muda mrefu inategemea kubeba taka
hizo kwa kutumia trekta moja ambalo ni chakavu.
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top