DIWANI wa kata ya mjini kupitia chama cha Demokrasia na
maendeleo (CHADEMA)katika Halmashauri ya
manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Joseph Fuime amemtaka mkurugenzi wa manispaa
hiyo kutoa ufafanuzi ambao unatumika kuchukuwa
fedha za mfuko wa Jimbo na zinatumika katika matumizi gani na wanafunzi
wanaosaidiwa kupitia mfuko huo ni wenye sifa zipi.
Hayo aliyasema jana wakati wa kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo ambapo alitaka
kujuwa maelezo ya wanafunzi 150 ambao wanasomeshwa na mfuko wa Jimbo baadhi yao kuto ripoti mashuleni kwa kigezo
cha kutolipiwa ada.
“Mwenyekiti naomba mkurugenzi alieleze baraza hili juu ya
mtiririko upi wa fedha za mfuko wa jimbo zinaletwa ,utaratibu gani unatumika
katika kuzileta hizo fedha na zikija zinaenda wapi maana kwenye makabrasha yenu
mmeandika kuwa zinalipia ada wanafunzi 123 wakati baadhi yao wapo tu majumbani
kwa sababu ya kukosa ada naomba majibu.”alisema Fuime.
Kwa upande wake meya
wa manispaa hiyo Charles Muhagama alisema kuwa fedha za mfuko wa jimbo
haziji kwa mtiririko wa aina yoyote ile isipokuwa zinaletwa kwa aajiri ya
maendeleo ya jimbo hata hivyo fedha hizo huwa zinachelewa kuletwa lakini watoto
hawajazuiwa kuripoti mashuleni.
Alifafanua zaidi kuwa zaidi ya watoto 150 wanasomeshwa na
mfuko huo waliopo kwenye mazingira magumu na kwamba fedha za mfuko wa jimbo kwa
mara ya mwisho zimeingia juni mwaka jana na kati ya watoto hao 123 wanasoma
sekondari,watoto wan ne wanasoma vyuo vikuu na 23 wanasoma vyuo mbalimbali.
Hata hivyo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dr.
Emanuel Nchimbi ambaye pia ni Waziri wa mambo ya Ndani kwa moyo wake wa
kuyelekeza fedha hizo zisomeshee watoto wasio na uwezo na wanaoishi katika
mazingira magumu kwani angeweza kuelekeza fedha hizo kwenye miradi mingine ya
maendeleo lakini kwa kutambua umuhimu wa elimu ameamua kuelekeza nguvu zake
kwenye elimu.
Post a Comment