Loading...

Breaking News:Maaskofu watoa tamko la amani tanzania, aliyemuuwa Padri akamatwa


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitafakari jambo            Dar es Salaam
WAKATI Jukwaa la Makanisa Tanzania (TCF) wakitoa tamko kali juu masuala mbalimbali yanayoashiria uvunjifu wa amani nchini Tanzania, kupitia kivuli cha dini mbili kubwa za wakristo na waislamu,Jeshi la polisi limemkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Erarist Mushi wa Kanisa Katoliki aliyeuawa Kisiwani Zanzibar.
Mtuhumiwa huyo amekamatwa eneo la Kariakoo Kisiwani humo na kupelekwa kituo cha Polisi kwa mahojiani zaidi.
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma Amon Kinyunyu akisoma tamko la Jukwa la Makanisa nchini alisema kwamba, Serikali inayoshindwa kulinda raia na mali zao haina sababu ya kung'ang'ania madarakani.
"Jukwaa la Makanisa ya Kikristo tumeazimia kuieleza serikali wazi juu ya matukio mbalimbali yanayotokea nchini, hususan yale yanayolenga kuuawa kwa viongozi wa dini, serikali kama imeshindwa kudhibiti hali hii haina sababu ya kung'ang'ania madarakani"alisema Askofu Kinyunyu na kuongeza.
"Makanisa tuko tayari kuwaambia waumini wetu na wananchi kwa ujumla juu ya uamuzi wa kuchukuwa juu ya serikali,tuko tayari kuitangazia umma na ulimwengu mzima kwamba serikali ya Tanzania ni serikali inayotesa waumini wake na haiheshimu uhuru wa kuabudu".
Jukwaa la Makanisa nchini wametoa tamko hilo wakati wa ibaada ya Ijumaa ya kuadhimisha kuteswa na kuuawa kwa Yesu Kristo inayoadhimishwa na waumini wa dini hiyo Dunia nzima.
Hata hivyo tamko hilo limekuja siku chache tangu Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kudai kwamba Jeshi la Polisi nchini linafuga uhalifu kwa kile alichosema kwamba limeshindwa kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

source: http://www.habarimpya.comPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top