Kundi moja la waasi katika
Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, limeuteka mji muhimu kusini mashariki mwa
nchi hiyo karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Duru zimearifu kuwa Jeshi lilijiondoa kutoka mji wa Bangassou bila pingamizi yoyote. Kundi hilo la Seleka
lilisaini mkataba na serikali mwanzoni mwa mwaka huu na likapewa
uongozi wa baadhi ya wizara kuu za serikali. Hata hivyo tangu wakati huo
limekuwa likilalamikia baadhi ya masuala linalodai kuwa hayajatatuliwa.
Seleka ni nani?
Seleka (jina hilo likimaanisha muunguano) liliteka miji mingi nchini humo na hata kutishia kuuteka mji mkuu Bangui. Walisaini mkataba na serikali mnamo Januari 11 katika mji mkuu wa Gabon Libreville chini ya utawala wa Francoise Bezize.Mkataba huo ulifanikishwa kwa upatanishi wa viongozi wa eneo hilo na uliunda serikali ya muungano wa kitaifa na sasa inaongozwa na kiongozi wa upinzani Nicolas Tiangaye.
Tangu kuundwa serikali hiyo Seleka wamekuwa wakitilia shaka nia ya serikali na kuilaumu kwa kuendesha serikali mbadala inayohujumu nafasi yao. Wametishia kujiondoa kutoka serikalini mara kadhaa.
Post a Comment