Zoezi lilianza jana kwa makadinali kutoka duniani kote kukusanyika huko
St. Peters Square kwa ajili ya kuchagua papa mpya atakayeliongoza
kanisa katoliki duniani. Hii ni kufuatia kujiuzulu kwa Papa Benedict XVI
kutokana na umri mkubwa.
Zoezi hilo halijafanikiwa katika
raundi ya kwanza baada ya moshi mweusi kuonekana jana. Hiyo ni ishara ya
kutopata papa mpya na mchakato unaendelea.
Mchakato wa kuchagua Papa mpya huanza kwa kukusanyika kwa makadinali
115 wenye umri wa chini ya miaka 80 kutoka duniani kote. Makadinali
hujifungia ndani bila mawasiliano yeyote na dunia, mpaka pale Papa
atakapopatikana. Baada ya sala na maombi, makadinali hao kila mmoja
hutakiwa kupendekeza jina moja la Kadinali ambaye wanadhani anafaa kuwa
Papa.
Ushindi wa Kadinali kuwa Papa unategemea zaidi ya 2/3 ya
mapendekezo yote, kwa maana hii, Kadinali anatakiwa kupata zaidi ya
mapendekezo 77 ili awe Papa.
Mchakato usipofanikiwa, karatasi
hizo za mapendekezo huchomwa kwa kemikali maalum ambazo husababisha
moshi mweusi, ishara kwa dunia ya kwamba bado Papa mpya hajapatikana.
Mchakato utaendelea mpaka pale dunia itakaposhuhudia moshi mweupe. Hiyo
ni ishara kwamba Papa mpya amekwisha patikana, na dunia ipo tayari
kumsikia.
Tunawatakia kila la kheri Kanisa Katoliki katika uchaguzi wa Papa mpya.
Like · · Share · 644
Zoezi lilianza jana kwa makadinali kutoka duniani kote kukusanyika huko St. Peters Square kwa ajili ya kuchagua papa mpya atakayeliongoza kanisa katoliki duniani. Hii ni kufuatia kujiuzulu kwa Papa Benedict XVI kutokana na umri mkubwa.
Zoezi hilo halijafanikiwa katika raundi ya kwanza baada ya moshi mweusi kuonekana jana. Hiyo ni ishara ya kutopata papa mpya na mchakato unaendelea.
Mchakato wa kuchagua Papa mpya huanza kwa kukusanyika kwa makadinali 115 wenye umri wa chini ya miaka 80 kutoka duniani kote. Makadinali hujifungia ndani bila mawasiliano yeyote na dunia, mpaka pale Papa atakapopatikana. Baada ya sala na maombi, makadinali hao kila mmoja hutakiwa kupendekeza jina moja la Kadinali ambaye wanadhani anafaa kuwa Papa.
Ushindi wa Kadinali kuwa Papa unategemea zaidi ya 2/3 ya mapendekezo yote, kwa maana hii, Kadinali anatakiwa kupata zaidi ya mapendekezo 77 ili awe Papa.
Mchakato usipofanikiwa, karatasi hizo za mapendekezo huchomwa kwa kemikali maalum ambazo husababisha moshi mweusi, ishara kwa dunia ya kwamba bado Papa mpya hajapatikana. Mchakato utaendelea mpaka pale dunia itakaposhuhudia moshi mweupe. Hiyo ni ishara kwamba Papa mpya amekwisha patikana, na dunia ipo tayari kumsikia.
Tunawatakia kila la kheri Kanisa Katoliki katika uchaguzi wa Papa mpya.
Wednesday, March 13, 2013
Post a Comment