Loading...

MBUNGE WA SONGEA MJINI AKABIDHI MAGARI MAWILI KWA WANANCHI WAKE



Na Nathan Mtega,Songea yetu

Mbunge wa jimbo la songea mjini mkoani Ruvuma  Leuindas Gama amekabidhi magari mawili kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa jimbo ilo ambayo ni gari kwa ajili ya kubeba wagonjwa na moja likiwa kwa ajilki ya kuwsaidia wananchi hao wa jimbo hilo wanapopatwa na matatizo ya msiba au kufiwa kama sehemu ya ahadi zake za kushirikiana na wananchi alizozitoa kwao wakati kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Akizungumza na wananchi katika uwanja wa Maji maji wa mjini Songea wakati akikabidhi magari hayo amesema kwa kutambua changamoto za kipato na kiuchumi kwa wananchi walio wengi wa jimbo hilo la Songea zinazowakabili na kwa kuzingatia ushauri alioupata wakati wa kampeni hizo za uchaguzi na baada ya uchaguzi ameamua kuekeleza kwa vitendo ushauri huo.

Amesema magari hayo aliyokabidhi kwa wananchi yanapaswa kutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo huku akiongeza kuwa wasimamizi wakuu wa magari hayo ni wenyeviti wa mitaa wakishirikiana na katibu wake ambaye anawafahamu wenyeviti wote wa mitaa wa manispaa ya Songea na anaamini hakutakuwa na udanganyifu wala ubadhirifu katika matumizi ya magari hayo.

Wakizungumza baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye hafla hiyo mbali ya kupongeza na kushukuru kwa uamuzi huo wa mbunge wameahidi kuhakikisha magari hayo yanatunzwa na kutumiwa kwa madhumuini yaliyokusudiwa ambayo yanailenga jamii yote ya wananchi wa Manispaa hiyo ya Songea.

Aidha akizungumzia adha inayolalamikiwa na wananchi walio wengi ya kufungwa kwa kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea kwa ajili ya kupisha matengenezo ambayo yamechukua muda mrefu na kuanzishwa kwa kituo kipya cha mabasi kilichopo eneo la Msamala hali ambayo imekuwa ikiwagharimu wananchi kiasi kikubwa cha fedha wanapohitaji kusafiri Gama amesema matengenezo ya kituo hicho cha awali cha mabasi yamekamilika na baada ya wiki moja kituo hicho cha awali kitazinduliwa.

Amesema baada ya kuzinduliwa kwa kituo hicho cha mabasi cha awali mabasi yatakuwa na njia mbili tofauti kwa ajili ya kuingia na kutoka kwenye kituo hicho ili kuepusha usumbufu kwa watumiaji wa usafiri huo na kuongeza kuwa kituo kipya cha mabasi cha Msamala kitaendelea kutumika kwa mabasi hayo kupitia na kuendelea na safari za kwenda nje ya mkoa au kuingia kuelekea kituo kikuu cha mabasi cha awali.



Post a Comment

CodeNirvana
Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top