Loading...

CCM SONGEA YAISHIKA PABAYA CHADEMA KAMPENI ZA UDIWANI MANISPAA YA SONGEA


Na Stephano Mango, Songea

WANANCHI wa Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wametakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi unatarajiwa kufanyika aprili mosi mwaka huu kwa kumchagua mgombea wa Chama cha Mapinduzi ili aweze kushirikiana na wananchi katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo

Wito huo umetolewa jana na Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Diwani wa Vitimaalum Manispaa ya Songea Genfrida Haule kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani kata ya Lizaboni uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Madizini

Haule alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kina hazina kubwa ya makada ambao wanaweza kuipeperusha bendera ya chama katika uchaguzi huu wa udiwani lakini kutokana na busara za viongozi wa Ccm na matakwa ya wananchi tumemteua George Oddo aweze kuwatumikia wananchi wa kata hii

Alisema kuwa awali Kata hiyo ilikuwa ina matatizo mengi sana katika sekta ya Afya, elimu, barabara, maji na masoko lakini kutokana na sera nzuri za Ccm kwa kupitia aliyekuwa Diwani wa Kata hii marehemu Said Ali Manya Serikali ya inayoongozwa na Ccm ilikuwa sikivu na ndio maana mnaona maendeleo makubwa katika Kata ya Lizaboni

Alieleza zaidi kuwa kuna baadhi ya kero bado zipo kwenye kata hii hivyo ni vema mkamchagua diwani kupitia tiketi ya Ccm ili aweze kumalizia ahadi na kero ambazo marehemu ally Said Manya aliziorodhesha kwa kuweka mikakati ya utekelezaji ili kuleta mabadiliko zaidi ya kimaendeleo

Naye Hamis Abdala Ally ambaye ni mmoja wa timu mahiri ya kampeni ya Chama cha Mapinduzi alisema kuwa wananchi wanapaswa wazipuuze kelele za wapinzani ambao kwao kuona damu inamwagika katika Kata ya Lizaboni kwao ni ushindi
Ally alisema kuwa Chadema wamekosa sera na umakini katika kampeni zao kwa kushindwa kueleza mambo ambayo yataweza kuwasaidia wananchi badala yao wanaendekeza fujo na matusi huku wakishabikia kwa nguvu ukubwa uvunjifu wa amani katika kata hiyo

“ Nimesikitika sana kuona viongozi wa Chadema wanafurahia kuona kuna kijana amepigwa panga na kujeruhiwa vibaya na ajali ya kugongwa kwa mtoto juzi na kudai kuwa kwa kuwa damu imemwagika sasa ndio dalili ya ushindi kwao jambo ambalo linatia shaka wananchi na kudhani kuwa wao ndio waliopanga uvujaji damu huo” alisema Ally

Alieleza zaidi kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefanya mambo mengi toka upatikana uhuru wan chi hii kwa kuwawezesha wananchi kupata barabara safi, maji safi na salama, elimu, afya, masoko, na uwezeshaji wa mitaji ya kiuchumi kwa kuzungumza na taasisi za fedha kupunguza masharti katika mikopo yao kwa wananchi

Alifafanua kuwa kupatikana kwa vitu hivyo ndiko kunakosababisha wananchi wapate ustawi wao na kuchangia kuleta maendeleo kusudiwa kwani watakuwa wamekombolewa kwa kiasi kikubwa sana na kwamba mapungufu mengine yanafanyiwa kazi kwani yanafahamika waziwazi

Alisema kuwa kwa kuwa Serikali iliyopo madarakani ni ya Ccm na iliwekwa na wananchi hivyo kuwasikiliza Chadema kuwa wataleta maendeleo ni uongo mkubwa na kitendo cha kuwapigia kura aprili mosi mwaka huu ni kutupa kura zenu na mtasimamisha maendeleo kwa kipindi kirefu

Alifafanua kuwa nyinyi wenyewe wananchi ni mashahidi hakuna mwaka ambao wananchi wamelima mahindi mengi kama mwaka jana lakini Serikali imeyanunua yote na mengine yanaendelea kupelekwa kwenye hifadhi ya chakula sasa hao wanaosema mbolea imechakachuliwa na kusema Serikali imeshindwa kununua mahindi wanapata wapi ujasiri kama sio kuwadanganya wananchi?

“ Eti Zitto Kabwe anafika nyumbani kwa watu badala ya kuuliza wenyeji, yeye anakurupuka na kusema hapa kuna matatizo ya wizi wa mbolea, mafuta ya jenereta za umeme hivyo ichagueni Chadema ili idhibiti hilo, sasa kama wao wanafahamu kuna wizi kwanini wasiiambie Polisi ili mwizi akamatwe badala yake wanataka udiwani kwani Diwani ni Polisi? Watadhibiti kwa njia gani? Kama sio wao ndio wanaofanya mchezo huo mchafu?”

Alisema kuwa hali ya umeme ni ya uhakika kwasababu kulikuwa na tatizo la kiufundi lakini tayari Shirika la Tanesco limeshafanya kazi yake na umeme unapatikana ambapo wananchi wanaendelea na shughuli zao za kujiingizia kipato ili kuyafikia malengo ya maendeleo

Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Ccm Wilaya ya Songea Mjini Zuberi Mtelela alisema kuwa wananchi mpigieni kura Oddo George ili aweze akaungane na madiwani wenzake ili aweze kutimiza ahadi ambazo tuliziahidi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010

Mtelela alisema kuwa mkiichagua Chadema licha ya kuwa mtakuwa mmepoteza kura zenu na kusimamisha maendeleo kwa miaka mitatu bali mtakuwa mmeongeza kikundi cha watu wenye fujo kinachoshabikia mambo mabaya kwa jamii ya Manispaa ya Goodluck Songea Mbanowa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Vijana Mkoa wa Ruvuma Mwajuma Rashid alisema kuwa Chadema wamejipanga kuleta vurugu siku ya uchaguzi na tayari wameanza kuwapiga na kuwatishia viongozi wa Ccm hivyo wananchi mkiwapa kura watu hao mtakuwa mnajenga kizazi cha vurugu na kukwamisha maendeleo yaliyopangwa katika kata ya Lizaboni

Rashid alisema kuwa sisi tumetulia lakini uvumilivu una mwisho wake na endapo mamlaka zinazo husika hazitadhibiti mwenendo huo ambao unahatarisha amani katika uchaguzi huo nasi tunaweza tukatumia nguvu zetu ili wapiga kura na wanachama wa Ccm wawe salama

Naye Mwenyekiti wa Ccm Manispaa ya Songea Hemed Dizumba alisema kuwa kazi kubwa inafanywa na wananchi wa Lizaboni ndio maana Chadema wana haha kwani tayari wenyewe wanajua kuwa ushindi kwao haupo

Dizumba alisema kuwa ushahidi upo wazi kutokana na maneno wanayowasema wenyewe kwasababu hizo mbwembwe walizonazo wameshagundua kuwa zinaletwa na washabiki wao kutoka Bombambili, Majengo, Mjini, Mfaranyaki, Misufini na Ruvuma lakini sisi tunazungumza na watu wa Lizaboni ambao ndio wapiga kura
Kwa upande wake mgombea udiwani kupitia Chama hicho Oddo George alisema kuwa uzuri wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi wananchi mmeuona hivyo hakuna sababu ya kuichagua Chadema katika uchaguzi huo

George alisema kuwa mipango ipo wazi kinachotakiwa ni wananchi kukubari april mosi mwaka huu kuwa inapaswa kuitekelezwa na Chama cha Mapinduzi kupitia Diwani wake ambaye ni mimi hivyo wananchi naomba kura zenu zote ili niweze kuibeba mikoba aliyoiacha marehemu Ally Said Manya mabaye alikuwa Diwani wa kata hii kupitia Ccm

Alisema kuwa kama kweli wananchi wa Kata ya Lizaboni mnaheshimu maendeleo mliosaidiana kuyaleta Kata ya Lizaboni na Marehemu Manya basi msipoteze kura zenu kwa kumchagua mgombea wa Chadema ambaye ameshaonyesha kuwa hana dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo watanzania



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top