Loading...

SUGU na RUGE wapatanishwa

Kwa wadau wengi wa muziki hapa nchini Tanzania wamekuwa wakishuhudia mvutana na msuguano mkali kati ya mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama SUGU na Ruge Mutahaba. Ruge Mutahaba ni mmoja kati ya wakuu wa kituo maarufu cha radio hapa nchini Tanzania Clouds FM. Minongono mingi iliyakuwepo hapa awali kuhusu sintofahamu ya wawili hao inasemakana ilitokana na Ruge kumzidi maarifa Sugu katika mradi wa malaria ambao Sugu alitafuta wafadhili waje Tanzania na mradi huo, hivyo kitendo cha Ruge kuzidi kete sugu ndio kilicholeta mtafaruku huo.

Vilevile inasemekana kituo hicho cha radio kilikuwa hakipigi nyimbo za msanii huyo (SUGU) siku za nyuma kwa kuwa msanii huyo sugu hakuwa tayari kuwa chini ya utawala wa kampuni hiyo.

Mara nyingi mbunge huyo amekuwa akitaoa shutuma nyingi kwenye kampuni ya Ruge kuwa wamejimilikisha studio iliyotolewa na rais wa nchi kwa manufaa ya kampuni yao. Kitu hicho kikasababisha wasanii wengi kuungana na kuanzisha kundi la kiuanaharakati kupinga kunyonywa, kundi hilo lililoitwa ANTIVIRUS liliongozwa na Sugu.

Leo ugomvi huo umemalizwa rasmi.

Pichani katika Sugu na Ruge wakipeana mikono pembeni kushoto mbunge Nchimbi na kulia ni Tundu Lissu baada ya kupatanishwa.Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top