Loading...

CHADEMA SONGEA YAIFYATUKIA SERIKALI UKOSEFU WA MADAWA KWENYE VITUO VYA AFYA



Na Stephano Mango, Songea

WATANZANIA wametakiwa kuidai Serikali huduma bora ya afya kutokana na maradhi yanayowasumbua katika jamii ili wananchi wawe na afya bora katika kutimiza wajibu wao wa kuijenga nchi yenye kufuata haki za binadamu bila upendeleo.

Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime akihutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa kampeni za udiwani wa Kata ya Lizaboni uliofanyika kwenye viwanja vya Pacha nne kata ya Lizaboni.

Fuime alisema kuwa inasikitisha kuona Serikali ya Chama cha Mapinduzi inashindwa kusimamia vema usambazaji wa madawa katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospital ili wananchi waweze kupata huduma stahiki za matibabu badala yake inajikita kufanya dhihaka na afya za watanzania kwa kugawa ovyo vidhibiti mimba.

Alisema kuwa afya ya binadamu ni suala nyeti sana na halihitaji usanii au ubabaishaji wowote ule kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha madhara makubwa kwenye jamii na kusababisha kujenga taifa lenye afya mgogoro kutokana na watu wake kutokuwa na afya njema.

Alieleza kuwa ukienda katika maeneo ya kutolea matibabu utakuta lugha chafu kutoka kwa madaktari, madawa na vifaa tiba hakuna lakini ukibahatika kuingia katika stoo ambazo zinapaswa kutumika katika kuhifadhi madawa katika maeneo hayo utaona kuna madawa mengi ya kuzuia ujauzito na kufunga uzazi ndio yamejaa utafikiri kuwa upatikanaji wa ujauzito ni homa.

“ Ni aibu kuendelea kuwa na Serikali inayoshindwa kuheshimu uhai wa watu wake na kujikita na mambo ya kuzuia binadamu wengine wasizaliwe huku watanzania wengine wengi wanakufa kutokana na njaa, ajali, homa na majanga mengine ambayo yanazuilika” alisema Fuime.

Alieleza zaidi kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa udiwani wa Kata ya Lizaboni na kata zingine nchi pamoja na uchaguzi wa Arumeru Mashariki ni vema mkawachagua wagombea wa Chadema ili waweze kushirikiana na wananchi wa maeneo husika kuleta maendeleo kusudiwa na huduma bora za afya.

Alisema kuwa wagombea wa CCM hawana sera mpya wala dhamira ya kweli ya kubadilisha maisha ya watanzania kwasababu hawana mipango ya utekelezaji kwa yale wayasemayo na ndio maana utawasikia wakijinadi kuwa mara wakichaguliwa watafanya hiki na kile badala ya kusema kuwa wamefanya hiki na kile na kimebaki hiki
Kwa upande wake mgombea wa udiwani wa kata hiyo Alanus Mlongo alisema kuwa wananchi mnafahamu uwajibikaji wangu toka nikiwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa kwa miaka 8 sasa hivyo naomba kura zenu ili niweze kuwatumikia kwa upana zaidi
MWISHO



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top