Na songeayetu.blogspot.com
Naibu katibu mkuu wa
Chama cha Demakrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma, mheshimiwa Zitto Kabwe amewahakishia wakazi wa manispaa ya Songea kumaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme ambayo kwasasa limekuwa kero kubwa wa wananchi wa manispaa hiyo kwakuwa lipo ndani ya uwezo wake.
Zitto aliyasema hayo jana jioni wakati akihutubia maelfu ya wapiga kura katika kata ya Lizaboni iliyopo ndani ya manisapaa ya Songea.Wananchi wa kata ya Lizaboni wanataraji kufanya uchaguzi mdogo ili kumpata diwani ambaye ataziba pengo la aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Manya.
Katika
hotuba yake mheshimiwa Zitto amewahakikishia wakazi wa Songea kuwa atahakikisha
wafanyakazi wa TANESCO ambao wamekuwa na tabia ya kuiba mafuta ya jenereta za
kuzalishia umeme wanachukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo ili
kuondoa tatizo la umeme linaloukabili mji wa Songea na viunga vyake.
Zitto alisema akiwa
mwenyekiti hesabu za mashirika ya umma atashughulikia tatizo hilo kwa kufanya
mambo mawili kwanza kwa kuwahoji kwanini umeme ukatike hovyo Songea? Pili matumizi
ya mafuta yanatumikaje? Kisha baada ya
hapo mtiti wake mtauona. Alisema kama ameweza kumshughulikia mkurugenzi wa
TANESCO Tanzania, kwa Songea itakuwa ni kitu kidogo kwake.
Katika kuondoa kabisa tatizo la umeme katika
mkoa wa Ruvuma alisema ujenzi wa mitambo mikubwa ya kuzalisha umeme kwa makaa ya
mawe inajengwa Mbinga yenye uwezo
wakuzalisha megawati 120 na mji wa Songea utapata kilovoti 220 pia katika
kufanya tatizo hili kuwa ndoto kabisa, mkoa wa Ruvuma utaunganishwa na gridi ya
taifa kutoka Makambako mkoani Njombe.
Aidha, Zitto Kabwe
alitoa onyo kali kwa IGP na RPC wa mkoa wa Ruvuma endapo wataendelea na mpango
wao wa kutaka kumletea zengwe mgombea wa udiwani wa kata ya lizaboni kuwa anatuhuma
zinazomkabili toka mwaka 1988, CHADEMA wameinasa barua waliyoandikiana wakuu
hao wa jeshi la polisi. Zitto amehoji iweje tuhuma hizo zifumbiwe macho toka mwaka
1988 walikuwa wapi wakati mgombea huyo alivyokuwa kiongozi wa mtaa kwa vipindi
viwili? Pia inasemekana katika barua hiyo diwani huyo anaundiwa zengwe
linaloonesha kuwa yeye alikuwa anachochea waendesha pikipiki waandamane na
kuleta fujo katika kipindi cha mauaji yaliyokea miezi michache iliyopita mjini
hapa. Zitto amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji
yaliyotokea na si kutishia raia. Katika kukomesha kabisa tabia hiyo inayotaka
kufanywa na polisi Zitto ameahidi kuipeleka barua hiyo bungeni.
Pia alisema kuna tetesi za jeshi
la polisi kuwa na mpango wa kuleta polisi wengine kutoka nje ya mkoa wa Ruvuma siku ya uchanguzi ili kuwadhibiti wananchi wa
Lizaboni washindwe kupiga kura siku ya uchaguzi kwakuwa sasa polisi wa Songea wengi
wanakinga mkono chama hicho.
|
Wanachama na wafuasi wa CHADEMA wakiandamana |
|
Waendesha pikipiki wakiwa katika maandamano |
|
Mamia ya Wananchi wakiwasili katika mkutano wa CHADEMA |
|
Mh. Zitto Kabwe akiwasili katika viwanja vya mkutano |
|
Mh. Zitto Kabwe na Mh. Chiku Abwao |
|
Mh. Zitto na Mgombea udiwani |
|
Makamu mwenyekiti BAVICHA akimwaga sera Songea |
|
Mh. Zitto akiunguruma jukwaani |
|
Mwanachama wa CCM akirudisha kadi ya CCM na kujiunga na CHADEMA |
|
Hata bibi nae alihama CCM na kujiunga na CHADEMA |
|
Balozi wa Mtaa kwa tiketi ya CCM nae ahamia CHADEMA |
|
Piga Kiberiti vikorokoro vya CCM |
Wednesday, March 28, 2012
Post a Comment