KAMATI iliyoundwa
na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuchunguza chanzo cha mauaji ya watu
waliouwawa kuhusiana na imani za kishirikina na kusababisha vurugu za watu
kuandamana na iliyopolekea mauaji ya watu wawili imekamilika.
Kamati hiyo
iliyoundwa na watu wanane ikiongozwa na katibu tawala msaidizi miundombinu
Severin Tossi ili Serikali iweze kuchukuwa hatua na kuhakikisha mambo kama hayo
hayatokei tena
Akitoa taarifa hiyo
Mwambungu alisema kuwa wale wote waliotuhumiwa kwenye mauaji hayo wamefikishwa
kwenye vyombo vya sheria.
Hata hivyo alisema
kuwa kamati hiyo imeshindwa kuthibitisha uvumi wa watu kumi na nne waliouwawa
kwa kuhusishwa na imani za kishirikina na kwamba tabia ya watu kueneza uvumi wa
uongo ni mbaya sana kwani inagharama kubwa kwa wananchi na kuongeza kuwa kamati
hiyo imefatilia na kupata taarifa kuwa hakuna mtu yoyote aliyenyofolewa viungo
vya siri .
“Naomba nitoe rai
kwenu kuwa tabia hii ya uenezaji wa uvumi ni mbaya sana kwa sababu inagharama
kubwa sana kwa wananchi ambao wanashindwa kufanya kazi zao za kila siku katika
ujenzi wa Taifa.”alisema Mwambungu.
Amesema,tayari
elimu kwa wananchi imeshatolewa na wananchi wameanza kufanya kazi ya ulinzi
shirikishi kwa kushirikiana na polisi kata ambapo kazi ya ulinzi na kwamba
mitaa yote ya Manispaa ulinzi umeimalishwa.
Mwambungu ameongeza
kuwa, kwa sasa hali ya utulivu na usalama katika mkoa wa Ruvuma imerejea kama
awali ambapo wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida .
“Napenda
kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Ruvuma na watu wanaoishi nje ya mkoa wa
Ruvuma kuwa Songea ni salama na wananchi wanaendelea na shuguli zao kama
kawaida, nawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa pia
wanahabari kwa kusaidia kurejesha hali ya utulivu na amani ”alisema
Aidha, amewataka
wananchi kuelewewa umuhimu wa kujilinda na kufata sheria ikiwa ni pamoja na
kuacha hulka ya kujichukulia hatua mkononi ,ikiwa ni pamoja na kuacha
kujihusisha na tabia za uvumi na hisia za kishirikina ili kuimarisha amani na
utulivu.
Post a Comment