Loading...

Tepe za HIV shuleni Tanzania zakera



Utepe mwekundu kuashiria maambukisi ya HIV
Wanaharakati nchini Tanzania wameelezea kughadhabishwa na hatua ya baadhi ya shule nchini humo kuwataka wanafunzi wanoishi na virusi vya HIV kuvaa riboni nyekundu kwenye sare zao za shule wakiwa shuleni.
Mwalimu mkuu wa shule moja ameambia BBC kuwa kitendo hicho kilifanyika kufuatia ombi la wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wagonjwa hawapewi majukumu ambayo huenda yakaathiri afya yao.
Lakini ubaguzi kama huu unakiuka sheria ambao adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu gerezani kulingana na shirika moja la kutetea haki za waathirika wa HIV.
Waziri wa afya amesema hawezi kutoa tamko lolote kuhusu madai hayo hadi uchunguzi utakapofanywa.
Kulingana na shirika la UNAids, takriban asilimia tano ya watu milioni 1.4 nchini Tanzania, wanaishi na virusi vya HIV.



Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top