WAKUU wa shule za msingi na sekondari zilizopo Hanga katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wakiongozwa na mkuu wa Seminari Hanga Fr JohnChrysostom Mukurasi, OSB wameanzisha siku ya kudumisha utamaduni (Utamadunisho) wa Kitanzania kwa kuwatumia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizopo katika eneo hilo na kuarika baadhi ya shule kutoka manispaa ya Songea. Tamasha hilo ambalo limelenga kurithisha utamaduni wa Kitanzania kwa watoto lilianzishwa mwaka 2010.
Akizungumza wakati wa kufungua Tamasha hili mkuu wa seminari ya Hanga Fr JohnChrysostom Mukurasi, OSB alisema utamaduni wa Kitanzania unaweza ukapotea kama hakutakuwa na jitihada za kurithisha utamaduni kwa watoto. Aliongeza kwa kusema endapo tutaboresha ngoma zetu na kuzitangaza nje ya Tanzania itakuwa ni njia nyingine ya kutangaza utamaduni wetu nje ya nchi yetu na kuongeza kipato, akitolea mfano ngoma za kusini mwa Afrika kama (Makhirikhiri) walivyoweza kutangaza utamaduni wao kimataifa.
Mgeni rasmi kutoka makumbusho ya Taifa ya Majimaji ndg. Bartazary alisema kitendo kilichofanywa na wakuu wa shule hizo ni cha kuigwa na kinafaa kiendelezwa na jamii nzima. Alisema kuandaa tamasha kama hilo ni gharama hivyo inafaa kutafuta wadhamini ambao watasaidia katika kuendesha matamasha kama hayo.
Shule zilizoshiriki katika tamasha hilo ni pamoja na DDC waliocheza ngoma ya Mganda, Hanga seminari walicheza ngoma ya Beta na ligui, Del Paul walicheza ngoma kutoka Ethiopia, St. Laurent walicheza ngoma ya wabena (kiduo), Coland walicheza Kioda, Bombambili walicheza Mkwaju ngoma. Shule nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Hoja sekondari na St. Benedick.
Wanafunzi wa shule ya msingi DDC wakicheza Mganda |
Wanafunzi wa Hanga Seminari wakicheza ngoma ya Beta |
Wanafunzi wa Del Paul wakicheza ngoma kutoka Ethiopia |
Wanafunzi wa ST. Laurent wakicheza ngoma ya Wabena (kiduo) |
Wanafunzi wa Coland wakicheza ngoma ya Kioda |
Hakika Tamasha lilifana
Wanafunzi wakishuhudia wenzao wakicheza ngoma
Wanafunzi wa Hanga Seminari wakicheza ngoma ya Ligui
Wanafunzi wa shule ya msingi Bombambili wakicheza mkwaju ngoma
Post a Comment