Loading...

Mkandarasi amvunja mguu polisi kwa risasi

Chanzo: Mwananchi                                                                                   Jumanne, 22 May 2012 20:07
 
Kwirinus Mapunda, Songea

MKANDARASI mmoja wa Manispaa ya Songea, Ruvuma (jina tunalihifadhi) anashikiliwa na Polisi mkoani hapa kwa tuhuma ya kumpiga risasi askari polisi na kumvunja miguu yote miwili.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa Ruvuma, George Chipos alimtaja askari aliyepigwa risasi kuwa ni Lucas Komba ambaye kituo chake cha kazi ni Mkoa wa Tabora. Alikuwa hapa kwa mapumziko na kwamba tukio hilo lilitokea Mei, 20 mwaka huu saa 2.45 usiku katika grosari iliyopo Seedfarm Barabara ya Namtumbo.

Chipos alisema mkandarasi huyo aliyepewa kazi ya kutengeneza Barabara za vijijini, alimpiga risasi askari Komba mwenye No.E 9507 PC kutokana na kile kinachodaiwa ni mtuhumiwa kulewa kupita kiasi hivyo kuanza kufyatua risasi hewani bila utaratibu.

Alisema askari Komba alishambuliwa baada ya kujaribu kumzuia. Alimfyatulia risasi miguuni na kumpiga sehemu ya paja la mguu wa kushoto.

Kaimu kamanda huyo alisema askari Komba amelezwa katika Hospitali ya Mkoa Ruvuma akipatiwa matibabu na mtuhumiwa atapandishwa kizimbani baada ya upelelezi kukamilika.

Katika tukio jingine: Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja, Esau Kapinga yaliyotokea katika Kijiji cha Mkumbi Wilaya ya Mbinga, Ruvuma. Marehemu aliuawa kwa kukatwakatwa kwenye goti la kulia na kupigwa na kitu kizito mgongoni.

Kamanda Chipos alisema tukio hilo lilitokea Mei 21, mwaka huu saa 7:00 usiku na kuwa chanzo chake ni ugomvi wa kifamilia wa kugombea mashamba ya kahawa. Alisema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top