Loading...

Tanesco Mkoa wa Ruvuma yaahidi umeme wa uhakika ifikapo juni 2012

Na. songeayetu.blogspot.com
Baada ya kilio na kero ya muda mrefu ya ukosefu wa nishati muhimu ya umeme mkoani Ruvuma hususan katika manispaa ya Songea, shirika la umeme nchini (Tanesco) limeahidi kutatua tatizo hilo sugu kutokana na mafundi kuthibitisha kutatua tatizo hilo. Mafundi waliopiga kambi kwenye kituo hicho cha kuzalisha umeme kilichopo maeneo ya Kiburang'oma wamethibitisha mbele ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Thabit Mwambungu aliyetembelea mitambo hiyo siku ya leo jumatatu ikiwa ni siku mbili tu baada ya Chama cha demokrasia na maendeleo kuitisha maandamano ya amani kupinga kero hiyo ambayo imeonekana kudumu katika kipindi cha miaka minne mfululizo.

katika kuthibitisha hilo, mkuu wa mkoa amesema kuwa anaamini kuwa kero hiyo itakoma ikiwa ni ahadi ya mheshiomiwa raisi wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete aliyeahidi kuleta mitambo mipya ya kufua umeme katika mkoa wa Ruvuma. Mafundi hao wamesema kuwa umeme wa uhakika utapatikana ifikapo mwezi juni kwani mahitaji ya umeme kwa manispaa ya Ruvuma ni Megawati 4.5 na ukarabati wa mitambo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme usiopungua Megawati 5.

kuhusiana na tatizo la mafuta, wamethibitisha kuwa mafuta yapo ya kutosha kuzalisha umeme. Kuhusiana na wizi wa mafuta wamesema hakuna wizi huo na kama upo basi ni wa ndani ambao wataendeleo kuchunguza.



2 comments

tutashukuru maana tumechoka na kauli zao na je ifikapo juni tatizo likaendelea tufanyeje maana hao watu kwa ahadi ndo zao

Reply

jamani juni si ndo hii umeme leo hakuna tufanyeje au ndo danganya toto?

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top