Loading...

UVCCM RUVUMA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA KUSUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI NA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA‏

Na Gideon Mwakanosya, Songea

JUMUIYA ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Mkoani Ruvuma imemwomba Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuendeleza zaidi kasi yake ya ya kuwawajibisha watendaji wezi ambao ni wabadhirifu wa mali ya umma kwa kuwa tabia hiyo ni kinyume ya maaadili ya uongozi .

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake katibu wa umoja wa vijana  wa chama cha mapinduzi  (UVCCM) Mkoani Ruvuma Mwajuma Rashidi  alisema kuwa jumuiya hiyo mkoa wa Ruvuma inampongeza Raisi Kikwete Kwa kitendendo chake cha ujasili cha kulisuka  upya Baraza lake la mawazili ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza manung’uniko ya watanzania wengi .

Alafafanua zaidi kusema kuwa Kikwete kutokana na kuusuka upya baraza lake la mawaziri UVCCM Ruvuma inampongeza sana kwa uondoa ukimya wa muda wa muda mrefu kufuatia kuwa uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya ama kwa akika kimya kingi kinamshindo mkubwa.

“Raisi kiwete UVCCM Ruvuma inampongeza wakuu wa wilaya wapya wakiwemo wanawake pamoja na vijana ambao wanatarajiwa kutoa mshango mkubwa sana katika vituo vyao vya kazi walivyo pangiwa alisema Katibu huyo wa UVCCM Mkoa Mwajuma”

Katibu huyo wa UVCCM Mkoa Mwajuma alieleza zaidi kuwa Rais Kikwete anaungwa mkono kwa asilimia 100 na jumuiya ya ummoja wa vijana wachama cha mapinduzi (UVCCM) na imemtaka afahamu kuwa Jumuiya hivyo iko pamoja na yeye katika vita ya kuwabana mafisadi wanao kula fedha za umma bila uoga.

Alibainisha zadi kuwa Rais Kikwete amewateuwa wakuu wilaya wapya na wakuu wengine wazamani waliobaki madarakani hivyo kila mmoja kwa wakati wake amepewa dhamana kubwa ya kwenda kufanya kwa kuzingatia maadili na uaminifu kwa hali wa ali ya juu kwenye kituo chake cha kazi alichopangiwa.

“wakuu wa wilaya wapya mulio teuliwa na wakuu wa wilaya muliokuwepo tangu awali amabao bado muko madarakani kwenye vituo vyeenu nendeni mukawajibike kwani inawezekana kutimiza wajibu wenu ili watanzania wakiwemo wanawake na vijana tusije tukamlaumu Rais Kikwete kwa mapungufu yenu bali kasi kubwa iwe kusimamia utekelezaji wa irani kwa ufanisi zaidi alisema katibu wa UVCCM Mkoa Ruvuma Mwajuma.”

Alisema kuwa UVCCM mkoa wa Ruvuma inamwomba Rais Kikwete aendelee kuwawajibisha wote watakao onekana kukichafua chama cha Mapinduzi mbele ya Umma ya watanzania kwa kuwaendeleza zaidi ufisadi wa mali za Umma na kukosa uwajibikaji, uwadilifu wa dhamana walizo pewa kujinufaisha wao wenyewe bila uoga.
Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top