Loading...

MGOMA WA WALIMU TANZANIA RIPOTI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI

Sasa hivi wanafunzi kata ya ilemela mkoa wa mwanza wapo katika maandamano wakiwa na mabango tofauti yenye maandishi "tunataka haki zetu" wakielekea mahakama ya mwanzo wilaya ya ilemela kufungua kesi zidi ya waalimu kwa kukataa kuwafundisha...

UPDATES:
TBC1 imeripoti kuwa Ruvuma walimu wamegoma na imethibitisha vurugu kutokea mkoani Mbeya na kuwa nako walimu wamegoma.

By MASIKITIKO:
Singida:

Wanafunzi wamekusanyika ofisi ya mkuu wa Mkoa muda huu mkoa wa Singida.

By agapetc:
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, walimu wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Korogwe wamegoma kwenda shule kwa kuunga mkono viongozi wao walioutangaza.

Shule nyingi zimeonekana walimu wakuu na wakuu wa shule tu ndiyo waliohudhuria maofisini, pia imebainika kuwa walimu wa sekondari wanaongoza kwa kutoenda kazini wakati shule za msingi imebainika walimu ktk shule chache wameenda kazini.

By Leonard Robert:
Huku Tanga wamefanya kweli, shule zilizonizunguka zote watoto wako wanacheza kaponda, hamna kinachoendelea, nimeongea na mwalimu mkuu mmoja hapa amesema kugoma kuko palepale na amesema leo hafungui hato ofisi..

Kama nchi nzima ni hivi basi walimu wameamua

By Steve1:
Iringa Mjini nako kimenuka, ni walimu wakuu peke yao wapo vituo vya kazi.

By mtendaji wa kijiji:
Huku Wilaya ya Same nako kimenuka.

Nimepita shule za Njoro, Ishinde, Majevu, Kisima, Makanya na Nkwini hakuna waalimu shuleni wanafunzi wametelekezwa

By Goldman:
Tunduma wanafunzi wakati wanaandamana, FFU wamewapiga bomu la machozi, sasa watu wakubwa wameingilia, gate la kwenda Zambia limefungwa kwa muda hakuna gari kuvuka!

By mpenda pombe:
Nipo huku Tabora, shule nyingi za mjini zimefungwa waalimu wamegoma, isipokua shule moja tu ya Msingi Mtendeni wapo waalimu wawili tu..

Nitaendelea kuwajuza..

By Micro E coli:
Na huku Tegeta, Boko kimenuka. Mfano, Boko Secondary - hakuna walimu waliofika.

By Kiumbo:
Kibaha Mlandizi shule karibia zote msingi na sekondari hakuna walimu kabisa. Wanafunzi wamefurahi leo utawala binafsi kutoroka wakati wenzao wanaandamana.

By :
Eddy Kinawiro huku Kimara wanafunzi wa Shule ya Msing Kimara B wamerudi wote kutokana na kuwa shuleni hakuna walimu

By KIFUBA KYA ITAHWA:
Huku Bukoba nako kimenuka nipo Bukoba mjini hakuna walimu walioenda kazini na sekondari ndo kabisa hazina watu

By nolakinabo:
Katika mkoa wa Kilimanjaro:

Katika shule za msingi walimu wakuu wameonekana wakiwahi shuleni huku wakiwa hawaelewi mgomo upo vipi "Mi siwezi kugoma nimebakiza mwaka mmoja kustaafu" mwalimu mkuu mmoja alisema.

Hali hii inaonekana kuwa mgomo huu hauna nguvu walimu wakuu wanawalazimisha walimu wao kufundisha..

Nako mkoani Arusha hali ni tete, nikiwa Karatu Mjini shule nazo hazina walimu, wanafunzi; wapo walimu wakuu hasa wale wenye umri wamekuwa waoga kugoma

By MotoYaMbongo:
Urambo Mkoani Tabora, wanafunzi za sekondari wamesambaa mitaani, wa shule za msingi wametawanywa na walimu wakuu wao.

By nachid:
Iringa naona watoto wapo mtaani wanaserebuka

By Gwaje:
Nipo Igunga hapa mjini, kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana

By summa:
DODOMA
walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa

By Barnabas Shadrack:
Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.

By Bajabiri:
Rafiki yangu ni mwalimu wa Halmashauri ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE

By Adolph:
Huku Kibaha napo kimenuka. Wanafunzi wamerudi majumbani kwao. Hakuna kinachoendelea!

By MotoYaMbongo:
Urambo Mkoani Tabora, wanafunzi za sekondari wamesambaa mitaani, wa shule za msingi wametawanywa na walimu wakuu wao.

Mgomo umefanikiwa, walimu kaza uzi.

By nachid:
Iringa naona watoto wapo mtaani wanaserebuka

By Gwaje:
Nipo igunga hapa mjuni kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana

By summa:
DODOMA
walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa
SOLIDARITY 4 EVER

By Barnabas Shadrack:
Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.

By Bajabiri:
Rafiki yangu ni mwalim wa halmashaur ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE

By Adolph:
Huku kibaha napo kimenuka..wanafunzi wamerudi majumbani kwao..hakuna kinachoendelea!

By samilakadunda:
Taarifa toka mkoa wa Morogoro:

Wanafunzi wanarudi nyumbani, secondary kwa Misinga wanafunzi wanazagaa mjini, hadi kieleweke, nimeongea na baadhi ya wanafunzi wanasema warudi nyumbani kwa kuwa waalimu hawapo mashuleni.

By :
Lucas Sabuni Baadhi ya S/M Nzega mjini wanafunzi wamerudi majumbani hakuna walimu mashuleni.

By Neiwa:
Upande wa Tunduma vurugu za wanafunzi zimetulia sasa (au niseme zimetulizwa); Hayo maandamano ya wanafunzi yalipelekea boarder ya upande wa Tunduma kusimamisha shuguli zake (sio kufungwa) kwa hofu ya usalama wa mali za wasafiri wanaotumia huo mpaka hasa magari ambayo huwa kwa wingi maeneo hayo.

Hata hivo so far shughuli zinaendelea kama kawaida kwa sasa katika offisi hizo za Migration hapo mpakani.

By msweken:
Mgomo hadi shule za vijijini kabisa, wife anafundisha mpwapwa kanambia mkuu wa shule pekee ndiye aliyeenda kituo cha kazi, walimu wengine wote hakuna aliyejitingisha, wapo makwao wanafanya mambo yao..!!

By Getsemane:
Mbozi:
Huku pia hapa Vwawa watoto wamegoma na wameandamana hadi kwenye ofisi za halmashauri(Bomani) ambapo pia ofisi za mkuu wa wilaya zipo. Mtaani pia watoto wamezagaa na wimbo wao ule ule "Tunataka haki zetu" wameongeza tena kuwa "Hatutaki kupewa rushwa"

By master gland:
Hapa mkoani Mtwara na wilaya zake zote ikiwemo Newala, Masasi, Tandahimba, Nanyumbu, Mtwara mjini hali ni tete hakuna walimu zaidi ya wakuu wa shule.

MAAFISA ELIMU WANARANDARANDA MASHULENI NA FORM ZAO NA WANAKOSA WAKUMSAHINISHA HALI NI TETE

By Echolima:
Niko Kahama mjini Mgomo wa waalimu unaendelea kama kawaida

By :
Simon Mwangoka Mwasile Shule ya secondary Uyole na shule ya msingi Itezi zilizoko katika jiji la mbeya wamegoma 99% nimeshuhudia mwenyewe kwa kutembelea maeneo husika.

By Mikael P Aweda:
Kisarawe, karibu shule zote hakuna walimu. Wanafunzi wanacheza shuleni.

Source: Mimi mwenyewe niko huku kikazi.

By Kengedume:
Nimezungu takribani shule kadhaa hapa ndani ya manispaa ya Shinyanga, mpaka dakika hii wanafunzi wametapakaa nje ya madarasa wanacheza tangu asubuhi! Shule ya msingi Ushirika, Bugoi, Chamaguha na n.k

Kimenuka mbaya!
chanzo jamiiforum.com bofya hapaPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top