Loading...

BREAKING NEWEEES: VURUGU ZA UHALALI WA KUCHINJA WANYAMA ZATOKEA TUNDUMA -MBEYA

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Tunduma Mbeya zinasema kumetokea vurugu kubwa baada ya wananchi wa pande mbili, Uislamu na Ukristo, kudai kila upande una haki ya kuchinja wanyama na kuuza katika bucha.

Shuhuda kutoka Tunduma ameiambia Blog hii kuwa chanzo cha vurugu hizi ni baada ya wakristo kuamua kuchinja wanyama na mtaalamu wa kukagua usalama wa nyama kuamua kupima nyama iliyochinjwa na Waislamu na kuiacha iliyochinjwa na Wakristo. 
Chanzo kiliendelea kusema baada ya Wakristo kuona nyama yao haijakaguliwa wakati nyama iliyokuwa imechinjwa na Waislam ikiendelea kuuzwa, Wakristo waliamua kuingia mitaani kushinikiza bucha za waislam zifungwe.
Hata hivyo, suluhu iliweza kupatikana baada ya kuruhusu nyama za Wakristo kupimwa na bucha zao kuendelea kufanya kazi.
"Nimeshuhudia bucha ya Wakristo ikifunguliwa na kuruhusiwa kutoa huduma kisha wakaelekea kufungua bucha nyingine katika eneo lingine" alisema shuhuda.
Katika vurugu hizi hakukuripotiwa maafa yoyote kutokana na askari kuchukua hatua za tahadhari zaidi wakati wa kutafuta ufumbuzi. 
"Nimemsikia diwani akisema msiwapige mabomu maana ni wao (Wananchi) wameamua" alisema shuhuda mmoja. 

Utulivu umeanza kurudi katika hali ya kawaida baada ya nyama zilizochinjwa na pande mbili kuruhisiwa kuuzwa.

"hapa nilipo pana bucha ya Wakrito naona wateja wanaingia kwa wingi muda huu na hakuna vurugu tena". Alisema shuhuda.
 Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top