Loading...

HOSPITALI YA SERIKALI YA MKOA YAKABILIWA NA UHABA WA VITENDEA KAZI


Hospitali  ya serikali ya mkoa wa Ruvuma inakabiliwa na matatizo makubwa ya uhaba wa vitendea kazi ikiwemo na uhaba wa mashine ya kuchemshia vifaa tiba.
Baadhi ya madaktiri wa hospitali ambao waliomba majina yao yahifadhiwe waliiambia NIPASHE kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na uhaba wa vitendea kazi na baadhi ya vitendea kazi vilivyopo vimechakaa na havifanyikazi kabisa jambo ambalo kwa limekuwa ni kero.

Walieleza zaidi kuwa hospitali hiyo imekuwa na tatizo kubwa la mashine ya x-ray ambayo kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo wagonjwa wengi waliokuwa wanatakiwa wapate vipimo kwa mashine hiyo wakuwa wakishauriwa kwenda kwenye hospitali ya misheni ya Peramiho ambako kuna huduma ya x – ray.
Madaktari hao waolewa meiomba serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kuona umuhimu wa kuwatafutia vitendea kazi haraka iwezekanavyo ili huduma ziweze kutolewa vizuri zaidi tafauti

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma Dr. Benedict Ngaiza alipohojiwa na NIPASHE juzi ofisini kwake kuhusiana na matatizo ya uhaba wa vitendea kazi kwenye hospitali hiyo alieleza kuwa mashine za kuchemshia viafaatiba zipo 4 lakini inayofanyakazi ni moja tu, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiharibika na kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara. Ambapo alitaja athari kubwa zitokanazo na tatizo hilo kuwa ni vifaa tiba vilivyoko kwenye kitengo cha maabara na chumba cha upasuaji haviwezi kufanyakazi hivyo huduma ya upimaji na upasuaji lazima isimame.
Dr. Ngaiza alieleza zaidi kuwa kuhusu mashine ya x-ray bado ni mbovu kwa muda mrefu pamoja na kwamba vyumba vya mashine ya x – ray vinaendelea kukarabatiwa.

Alisema kuwa changamoto kubwa ni kwamba baadhi ya huduma zinazohusisha uchunguzi zaidi ya x ray zimesimamishwa na huduma hiyo imekuwa ikipatikanaa katika hospitali zote za serikali za wilaya ambako kuna mashine za x – ray, alizitaja kuwa ni hospitali ya serikali y wilaya ya Mbinga na Tunduru. Na kwamba wagonjwa wanaofika kwenye hospitali ya serikali ya mkoa kwa ajili ya huduma ya x-ray hushauriwa kwenda kwenye hospitali ya misheni ya Peramiho ambako kuna hudama hiyo lakini nayo inaubovu kwani haifanyikazi kwa kiwango kinachotakiwa.
MWISHOPost a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright songeayetu.blogspot.com | Designed By JUNGUKUU.US
Back To Top