wachezaji wa mpira wa pete kutoka chuo cha TEKU kabla ya kuanza mchezo
wachezaji wa SAUT na TEKU wakiendelea na mchezo wa mpira wa pete
wazezaji wa volleyball wakipambana katika uwanja wa zimanimoto
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wakifuatilia pambano
kabla ya kuanza mchezo
wachezaji SAUT
wachezaji TEKU
mashabiki wakishuhudia upigaji wa penati
WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) kutoka mkoani Mbeya wameweza kuichapa timu ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Mt.Agustino tawi la Songea kwenye mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu uliofanyika katika uwanja wa Majimaji uliopo kwenye manispaa ya Songea.
Mchezo huo ulitanguliwa na michezo mingine ambapo awali kulikuwa na mchezo wa pete kwa wasichana ambapo TEKU waliweza kuilaza timu ya wasichana kwa jumla ya alama kumi na mbili kwa alama saba, huku mchezo mwingine ulikuwa ni mpira wa wavu ambapo SAUT waliweza kuishinda licha ya kupoteza michezo mingine miwili japokuwa wao wakiwa wenyeji wa mchezo huo.
Kwa upande wa mpira wa miguu, katika muda wa dakika tisini wachezaji hao waliweza kutoka bila kufungana na baada ya wachezaji hao kuhitaji mshindi apatikane ndipo walipoamua kupigwa kwa penati ambapo wachezaji wa SAUT waliweza kupoteza penati tatu huku TEKU wakipoteza penati moja kati ya penati tano zilizopigwa.
Post a Comment